Kama mbavyo tumezoe, mgawanyo wa majukumu hayo hufanywa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali kama vile umri pamoja na jinsia.
Kwa upande wa umri watu katika jamii nyingi hugawanywa katika makundi matatu. kundi la kwanza ni lile ilinaloanza na umri kuanzia miaka 0-7, kundi hili katika jamii huwa hawapewi majukumu ya aina yeyote, kundi la pili ni lile linaloanza na umri kuanzia miaka 7-14, na kundi la tatu na la mwisho ni lile linaloanza na umri kuanzia 14-18 na kuendelea hufahamika kama watu wazima.
Katika mada hii, napenda tuzungumzie kidogo juu ya kundi hili la pili ambalo pia linafahamika kama kundi la kati . Kundi hili kama ambavyo linaonyeshwa kwenye picha hapo juu, katika jamii nyingi huwa wanapangiwa yale majukumu madogo madogo ya nyumbani kama vile; kuosha vyombo, kufagia, kuchota maji n.k ukiachilia mballi majukumu mengine kama ya kusoma.
Katika hatua hii ya ukuaji, ni hatua ambayo ni muhimu sana kwa kuwa ni hatua ambayo mtoto hupata fursa nzuri ya kujifunza kati ya mambo mazuri na mambo mabaya kulingana na familia ambayo imemkuza. Kama wazazi na walezi watatimiza majukumu yao ya malezi kwa kuwafundisha watoto juu ya majukumu yao kama ambavyo imeelezwa kidogo hapo juu, basi kwa hakika tutapata watoto wanaojielewa na wenye uwezo wa kujitegemea.
Lakini kwa bahati mbaya ni kwamba mgawanyo huu hufanyika zaidi kwa ufasaha sehemu za kijijini ukilinganisha na sehemu za mijini. Watoto wengi wanaoishi mijini hasa wale ambao wanatoka katika familia mambo safi, wao haya mambo hawajui kabisa! Wengi wao huwachwa tu wamekaa kibwenyenye huku wakiwa chini ya uangalizi wa karibu wa wafanya kazi wa ndani. Watoto hawa mara nyingi huanza shule wakiwa na umri mdogo sana mfano,miaka mitatu, wakirudi nyumbani kutoka shuleni, kazi zote hukuta zimefanywa na wafanyakazi wa nyumbani. Ukweli ni kwamba elimu ya shule ni muhimu sana, lakini pia elimu ya maisha ni nzuri sana! (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment