BARCA.
| Jordi Roura. |
Kocha msaidizi wa klabu ya FC
BARCELONA, JORDI ROURA, ametoa pongezi za dhati kwa mwanasoka
bora duniani LIONEL MESSI baada ya kuisaidia timu yake kufunga goli la
kusawazisha kwenye mtanange wa kuwania
kufuzu hatua ya nusu fainali ya ligi ya bingwa
barani ulaya dhidi ya PSG ya nchini ufaransa
uliyopigwa hapo jana dimbani Nou Camp.
MESSI ambaye alishuka dimbani kipindi
cha pili akitokea benchi, aliweza kubadili sura ya mchezo kwa upande wa timu yake na kuisaidia timu hiyo kupata bao la kusawazisha
baada ya kutoa pasi maridadi iliyokwenda
moja kwa moja kwa DAN ALVES na baadaye kutiwa kambani na mshambuliaji
PEDRO mnamo dakika ya 71 ya mchezo.
Goli la vinara wa ligi kuu nchini
Ufaransa PSG lillisukumizwa nyavuni na
mshambuliaji hatari PASTORE mnamo dakika ya 50 ya mchezo,
Mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta ni kuvute ulimalizika kwa sare ya goli 1-1 na
kusababisha FC BARCELONA maarufu kama WAKATALUNYA kufuzu kuingia hatua ya nusu fainali katika michuano hiyo
Kutokana na sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo wa awali nchini Ufaransa.
PSG
| Ibrahimovic. |
Mshambuliaji
wa zamani wa klabu ya FC Barcelona anaye kipiga PARIS
SAINT GERNAIN kwa sasa,
ZLATAN IBRAHIMOVIC ameliambia shirika la habari la CNN kwamba,
anaheshimu uwezo wa kocha wa zamani wa klabu ya FC BARCELONA , PEP GADIOLA,
licha ya tofauti zao akiwa uwanja Nou Camp.
IBRAHIMOVIC amefunguka na kusema kuwa sababu
kubwa iliyomfanya kukimbia uwanja NOU
CAMP na kujiunga na klabu ya AC MILLAN kabla ya kuhamia klabu PSG mapema msimu huu ni kocha huyo maarufu kama madini
yanayotembea.Mchezaji huyo ameendelea kusema, pamoja na watu wengi kusifu uwezo wa GADIOLA kufundisha soka, kwa upande wake ametamba kuwa JOSE MORINHO na FABIO CAPELLO ambao ni makocha wake wa zamani akiwa MILLAN na JUVENTUS ndiyo wakufunzi wa soka aliowahi kukaa nao na kukubali kazi zao kuliko PEP GADIOLA.
LIVERPOOL.
| Ibe. |
Chipukizi huyo wa pembeni mwenye umri wa miaka 17, alijiunga na majogoo wa jiji akitokea klabu ya WYCOMBE na sasa anaonyesha soka la hali ya juu klabuni hapo.
Wakati kinda huyo akiendelea kufanya vizuri, naye kocha msaidizi wa kalbu hiyo ALEX INGLETHORPE , ameeleza kuwa kinda huyo amekuwa akimsumbua mara kwa mara akitaka video mbalimbali za Ronaldo.
Frrancis Kivuyo Baraka Mpenja Goal.com
0 comments:
Post a Comment