Bado suala la ubaguzi wa rangi kati ya watu wenye ngozi nyeupe(wazungu) na wenye ngozi nyeusi (wa Afrika) ni tatizo kubwa duniani, na mra nyingi tatizo hili limekuwa likionekana zaidi kwa wachezaji wa soka wa kiafrika wanaosakata kabumbu huko barani ulaya.
Kwa hara haraka, miongoni mwa wachezaji wa kiafrika waliokumbana na ubaguzi wa rangi tangu msimu huu uwanze ni Mari Baloteli (AC Millan) na Yaya Toure (Man City) japo kwa Toure siyo ya moja kwa moja.
Cha kusikitisha ni kwamba licha ya shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, kulikemea hili suala kwa nguvu zote bado makali yake yanaendele kupanda siku hadi siku.
Jana (Aprilli 27,2014) wakati Villareal wanacheza na Baselona FC, kituko kingine cha ubaguzi wa rangi kiliweza kushuhudiwa baada ya shabiki mmoja wa Villareal kunaswa na kamera za uwanjani akimrushia ndizi mchezaji wa Barcelona, Dani Alves wakati akijianda kucheza mpira wa kona kuelekea lango la Villareal.
| Hii ni video inayo muonyesha Dani Alives akibugia ndizi aliyorushiwa na mashabiki wa Villareal (video: Fox) |
Dani Alves hakushutushwa na kitendo hicho na alicho kifanya ni kuchukua hiyo ndizi na kuimenya kisha katupia mdomoni na kuimeza bila wasiwasi wowote.
''Tumekuwa tukisumbuliwa na matatizo ya ubaguzi wa rangi hapa Hispania kwa muda mrefu sasa. Lazima tujibu mapigo yao kwa njia ya mzaha zaidi, Ni vigumu kuliondoa suala hili kirahisi'' Alves alisema mara alipo ulizwa kuhusu suala hilo.
Katika mchezo huo Barcelona waliibuka na ushindi wa magoli matatu kwa mawili, magoli mawili ya Barcelona yalipatika kwa wachezaji wa Villareal kujifunga wenyewe huku Lionel Messi akiifunga goli la tatu nal ushindi mnamo dakika ya 77 ya mchezo huo.Sasa Baselona wanakuwa ktika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Hispania wakiwa point 84, point 4 nyuma ya vinara wa ligi hiyo kwa sasa Atletical Madri wenye point 88.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment