Kocha mkuu wa bingwa mtetezi waligi kuu Tanzania Bara Azam FC, "Mcameroon" Joseph Omog amesema vita ni mbinu na mbinu mojawapo kubwa ya kumshinda adui yako ni pamoja na kufahamu ubora wake na udhaifu wake hususani pale anapokuwa katika vita na ndiyo maana amewaruhusu wanandinga wake kuhairisha mazoezi ya jioni ili kupata nafasi ya kwenda uwanaja wa taifa leo Sep 6, 2014 kumshuhudia mpizani wake Simba Sc akimkabili Gormahia Fc kutoka nchini kenya ambaye ndiye kinara wa likuu nchini Kenya kwa sasa.
Hili siyo jambo la ajabu sana kwa makocha kutumia fursa ama mbinu kama hizi kuwasoma wapinzani wake, lakini ajabu katika hili la Josep Omog ni kurusu hata wanandiga wake kuhairisha mazoezi na kwenda uwanja wa taifa kushuhudia mechi ya hiyo ya leo, mimi binafsi kitendo hiki kwangu ni cha mara ya kwnza kuona na kusikia kocha na kiosi chake wanaenda uwanjani kumsoma mpinzani wakeke, ingawaje kwangu mimi naona ni mbinu nzuri sana.
Omog amesema kesho pia Sep 7, 2014 yeye na wachezaji wake watakuwepo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kufutilia mchezo mwingine kati ya Dar Young Africans dhidi ya Big Bullet kutoka nchini Malawi ambayo yenyewe ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini Malawi. (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:
Post a Comment