Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Costal Union Fc, Dr. Ahmed Twaha akiwa na kocha mpya wa klabu hiyo, James Nandwa ambaye amechukuwa nafasi ya Yusuph Chippo. |
Aliye wahi kuwa kuwa Kocha wa Kiungo Mkenya,
Victor Wanyama anayechezea soka lake kwenye klabu ya ,Southampton
nchini Uingereza James Nandwa ameingia mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha timu
ya Coastal Union ya Tanga.
Kocha
huyo anachukua mikoba iliyoachwa na Kocha Yusuph Chippo aliyekwenda nchini kwao
Kenya kutokana na matatizo ya kifamilia kuwa kwenye hali ambayo sio mzuri jambo
ambalo lilipelekea kushindwa kurejea
nchini kwa ajili ya kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Akizungumza
mara baada ya kutua jijini Tanga leo ikiwemo kulakiwa na viongozi wa klabu
hivyo wakiongozwa na Meneja wake ,Akida Machai wakiwemo Katibu Mkuu pamoja na
wajumbe wa kamati ya utendaji,Kocha huyo alisema kuwa dhamira yake kubwa ni
kuhakikisha anaipa mafanikio timu hiyo.
Akizungumza leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa ujio wa kocha
huyo utawezesha timu hiyo kufikia malengo yao ambayo wamejiwekea ya kuhakikisha
wanachukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Assenga amesema kuwa kutokana na uzoefu aliokuwa nao kocha
huyo utawezesha kupelekea chachu kwa wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho
kupambana wakiwa na lengo la kuipa mafanikio timu hiyo.
Kwa upande wake,Kocha Nandwa amesema kuwa kitu cha kwanza ni
kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yake iliyojiwekea ya kuwa timu bora
Tanzania ili iweze kupata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya kombe la
shirikisho.
“Kwanza nashukuru kupata nafasi ya kuifundisha Coastal Union
nitahakikisha nitaifikisha timu hii kwenye malengo waliojiwekea ya kuchukua
ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara kutokana na uzoefu wangu niliokuwa nao “Amesema
Nandwa.
Kocha Nandwa aliwahi kuzifundisha
timu za soka za Harambee Stars,AFC Leopard ya Kenya pamoja na Utalii ya Kenya
na kuipa mafanikio makubwa ikiwemo Ubingwa wa Ligi kuu nchini humo.
0 comments:
Post a Comment