Jumuia ya makocha nchini Uingereza leo imemtangaza  Kocha wa klabu ya Machester United Sir Alex Furguson kuwa kocha bora wa mwakaka wa ligi kuu nchini humo baada ya mechi yake ya mwisho dhidi ya WEST BROM iliyochezwa jumapili iliyopita.

Sir Alex Furguson.
Ferguson, ambaye  anastaafu kazi ya ukocha katika klabu ya MAN U baada ya kuifundisha klabu hiyo kwa muda wa miaka 26, sasa anakuwa ni meneja wa kwanza kuwahi  kushinda tuzo hiyo kwa mara ya nne.
Sir Alex Ferguson: Celebrates the Premier League title
Wapili kulia, Furguso na baadhi ya wachezaji wakishangilia ubingwa ligi kuu.

Akikabidhiwa zawadi hiyo na  meneja wa klbu ya West Ham  Sam Allardyce jana jioni, Furguson alikaririwa akitania kuwa kocha wa  West Brom Steve Clarke naye anastahili pongezi baada ya kufanikiwa kutoa sare ya magoli 5-5 dhidi ya Manchester United





GALATASARAY.

Mshambuliaji nguli wa zamani wa klabu CHELSEA lakini anayekipiga kwa sasa katika klabu ya Galalatasaray DIDIER DROGBA amepeleka malalamiko yake kwa waziri wa michezo  nchini ya Uturuki Suata Kilic baada ya  ya mashabiki wawili wa klabu ya FERNABAHCE  kuonekana wakibeba michora ya ndizi ambayo alidai ililenga kuonyesha hali ya ubaguzi wa rangi dhidi yake wakati Galatatasaray ikicheza dhidi ya klabu hiyo jijini INSTBUL May 12, mwaka huu

Drogba denies racist chanting will force him out of Turkey
Wapili kutoka kulia, Didier Drogba.

 Akiongea na waandishi wa habari, Drogba amesema licha ya kushitaki juu ya vitendo hivyo kwa waziri wa michezo nchini Uturuki, kamwe vitendo hivyo  haviwezi kumfanya aondoke nchini  Uturuki kwani anapenda kucheza soka huko, lakini pia anachukulia vitendo hivyo kama sehemu ya changamota katika kazi yake.

Lakini kwa upande wake SUAT KILIC amewasisitiza wadau wote wa soka kutotafisiri vibaya   kitendo cha mashabiki wa FC Fenerbhace kuja uwanjani na michoro ya ndizi kwani michoro hiyo inaweza kuwa na tafsiri nyingine zaidi  tofauti na hiyo.



UJERUMANI

Mshambuliaji wa klabuya BORUSSIA DORTMUND, Jakub Blszczykowski amesema ana imani kubwa kuwa klabu yake itaibuka mshindi dhidi ya FC Bayern kwenye fainali ya klabu bingwa barani ulaya itakayochezwa May 25 mwaka huu.


Kuba: Dortmund know how to beat Bayern
Jakub
Akiongea na mtandao wa UEFA, mapema leo hii Jakub amesistiza kuwa ushindi katika fainali ya ligi ya Mabinwa kati ya BORUSSIA DORTMUND na Bayern Munich itakayochezwa dimbani WEMBLEY , itategemea hali ya timu yenyewe siku hiyo, na timu yake imejipanga vilivyo kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
 
Lakini kwa upande wake beki wa kulia wa Bayern Munich Philipp Lahm, alisema  ubingwa wa Bundesliga waliochukuwa msimu huu, kamwe hautapunguza kasi yao ya kujiandaa na fainali ya klabu bingwa,
 
Lahm: Bayern hungry for success
Philipp Lahm
  huku akisisitiza kuwa timu yake iko fiti na wanasubiri kwa hamu kubwa fainali hizo.



(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top