Shirika la taifa la wakimbizi nchini Rwanda limesema linajipanga kuchunguza maombi
yote ya waasi wa zamani wa M 23 kutoka Demkrasia ya Congo ambao wameomba hifadhi
nchini humo baada ya kutangaza kuachana na shughuli zote za uasi.
Akiongea na vyombo mbalimbali vya habari nchini
Rwanda; Waziri anayesimamia masuala ya majanga na wakimbizi, Seraphine
Mukantabana amesema waasi hao wa zamani wa
M23 watapewa hifadhi nchini Rwanda mara baada ya shirika linaloshughulikia
masuala ya wakimbizi nchini humo kufanya uchunguzi wa kina juu ya maombi yao.
![]() |
Seraphine Mukantabana |
Seraphine Mukantabana ameeleza kuwa tayari wamewapatia waasi hao wa
zamani wa M23 fomu za kujaza ili kuzibitisha maombi yao, lakini bado
hawajarudisha fomu hizo mpaka sasa.
![]() |
M23 wakiwa katika harakati mbalimbali |
Aidha, kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa kundi hilo la zamani la M23 zinasema kuwa waaasi
hao kwa sasa wanataka kutambuliwa kama wakimbizi kwani kwa sasa hawajihusishi
na shuhuli zozote za kivita wala siasa.
Hata hivyo mwezi May mwaka huu waasi hao wametangaza
kuachana na masuala ya uasi katika mkutano wa kidipolomasi ulifanyika nchini
Rwanda pamoja mashirika ya kimataifa
yaliyowatembela kwenye kambi ya wakimbizi ya Goma iliyoko jimbo la Kaskazini mwa nchi ya
Rwanda.
Chanzo: The New Times [Rwanda
Online English newspaper]
MICHEZO
Hatimaye rais wa klabu ya
Paris St Germain, Nasser Al-Khelaifi
ametupilia kapuni tetesi zinazodai kuwa
mwanasoka Thiago Silva yuko mbioni kujiunga na miamba ya soka wa hispani a FC
Barcelona
Akiongea na vyombo mbalimbali
vya habari nchini Ufaransa Nasser
Al-Khelaifi amesema kwa sasa hawako
tayari kumuachia Thiago Silva kujiunga na klabu yoyote hadi mkataba wake na
klabu PSG itakapo kwisha.
![]() |
Pichani mwenye jezi nyeusi ni Thiago Silva |
Nasser Al-Khelaifi amesisitiza
kuwa bado PSG isingewza kupokea dau la Euro milioni 32 zinazodaiwa kutolewa na
klabu ya Wakatalunya kwani bado PSG inauhitaji mkubwa na nyota huyo kwa sasa
kwa kuwa mchezaji huyo ameendelea kuwa
na msaada mkubwa klabuni hapo.
Hata hivyo kwa mujibu wa maneno ya Thiago Silva
mwenye asili ya huko nchini Brazil; amesema
ni kweli kuwa kocha wa klabu ya FC Barcelona Tito Vilanova msimu
uliopita alimuambia kuwa anataka kumsajili katika klbu yake.
Chanzo: SKY SPORT
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment