Wa kwanza upande wa kulia kati ya walio simama ni "Julio" akizungumza na wachezaji wa Costal Union wakati wa mazoezi.
Baada ya kipigo cha magoli 8-0 kutoka kwa Yanga Sc jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kila mtu alikuwa na hamu ya kusikia atakacho kisema kocha wa Costal Union, Jamhuri Kihwelu "JULIO". Naamini ilikuwa ni wakati mgumu sana kwa Julio kuzungumza na waandishi wa habari, tena wenye kuuliza maswali ambayo muda mwingine yana maudhi.

Nikiwa nyumbani nilimsikia Julio akihojiwa na mwandishi wa kituo kimoja cha redio uwanja wa taifa baada ya mchezo huo ambapo licha ya Julio kujitahidi kuwa makini katika kuzungumza, bado niligundua hoja zake zilikuwa na madhaifu kiasi fulani.

"Unajua sisi baada ya mechi yetu dhidi ya Tanzania Prisons ambayo tulifungwa goli 1-0, tuliamua kupumzika kidogo na wachezaji wakaruhusiwa kwenda manyumbani kusheherkea sherehe za pasaka huku tukisubiri mechi yetu nyingine dhidi ya JKT Ruvu. Lakini cha kushangaza nikiwa nyumbani kusheherekea pasaka, nilipigiwa simu na kupewa taarifa kwamba mechi yetu dhidi ya JKT Ruvu imehairishwa na badala yake tutacheza na Yanga Sc tarehere 8-04-2015.

Sasa angaliam,wachezaji wanatoka likizo wanakuja kukutana na timu ya Yanga ambayo ilikuwa katika mashindano ya kimataifa, Yanga ambayo imepata  mazoezi ya kutosha na morali yao pia bado ipo juu. Costal Union ingeepukaje kipigo kama hiki?" Julio alisikika akijitetea.

Kwa mtazamo wa haraka hoja za Julio bado hazina ushawishi ukizingatia siyo mara ya kwanza Costal Union wanakutana na Yanga Sc,na wala siyo mabadiliko ya ratiba tu pekee inaweza kupelekea Costal Union kukubali kipigo cha magoli mengi ya kihistoria namna hiyo, lazima kutakuwa na kitu nyuma ya pazia.

Muda mfupi uliopita, Costal Union wamejikuta wakifanya mabadiliko ya mara kwa mara ya benji la ufundi hususani makocha. Mkenya Yusuph Chipo aliyekuwa na Costal Union kwa msimu wote uliopita kaondoka kwa njia ya kutatanisha, James Nandwa aliyeridhi mikoba ya Chipo naye kaondoka hivyohivyo, sasa Julio ndio kaachia usukani ambaye naye sina uhakika kama ataduma kwa hali ilivyo sasa klabuni hapo.

Kwa kutumia kigezo cha hapo juu peke yake unaweza ukagundua kwamba kuna mambo mengi makubwa na mazito ambayo siyo mazuri yanayoendelea katika klabu ya Costal Union. Ni sawa na kusema  Costal Union ni kama wanajichimbia kaburi lao wenyewe!




(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top