ALIYEKUWA Kocha wa makipa wa timu ya Yanga Razack Siwa hatimaye ameingia mkataba wa kuwanoa makipa wa timu ya Coastal Union ya Tanga ambayo inajiandaa na maandalizi ya msimu ujao wa Ligi kuu Tanzaniabara utakaoanza Mwezi ujao hapa nchini.
| Razack Siwa. |
Tayari Kocha Siwa ameungana na wachezaji wa timu hiyo leo kupanda ndege kuelekea Visiwani Pembaambapo timu hiyo inakwenda kuweka kambi ikijiwinda na michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
Akizungumza kabla ya timu hiyo kuondoka ,Katibu Mkuu wa Coastal Union ,Kassim El Siagi amesema kuwa kocha huyo wa makipa anachukua nafasi iliyokuwa wazi kutokana na kutokuwa na mwalimu maalumu wa kuwafundisha walinda milango wa Coastal Union.
Akizungumzia safari ya timu hiyo, El Siagi alisema kuwa safari ya timuhiyo leo wameondoka na wachezaji 27 wakiambatana na walimu wa timu hiyo ambao wameondoka ambapo watakapofika pemba watafanya mazoezi kwenye uwanja wa soka Gombani.
Safari hiyo imefadhiliwa na wadhamini wa timu hiyo kiwanda cha Pemba Floor Mils kilichopo mjini Tanga ambao wamedhamiria kuhakikisha wanaipa mafanikio timu hiyo.
Katibu huyo amesema wakiwa visiwani humo watacheza mechi nne zamajaribio ambazo zilikwisha kutayarishwa na chama cha mpira wa miguu Pemba pamoja na kuwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuacha kuwa na wasiwasi na timu hiyo kwa sababu wamefanya usajili wa nguvu . (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment