![]() |
Koscienly akiwa amevalia "Cap" kwa ajili ya kulinda jeraha lake baada ya kugonga kichwa na mshambuliaji wa Leicester, Jeffrey Schlupp |
Taarifa katoka shirikisho la soka nchini Ufaransa zimedhibitisha kuwa beki huyo kwa sasa hayupo katika hesabu ya wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa kinachotarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki siku za karibuni kati Hispania na Serbia.
Nafasi ya Koscienly kwa sasa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa inaonekana kuchukuliwa na beki anayekipiga kunako klabu ya Barcelona Jeremy Mathieu.
Mathieu, amejiunga na Wakatalunya msimu huu akitokea Valencia na amekwisha fanikiwa kucheza michezo miwili ya kimataifa.
Kitengo cha utabibu ya klabu ya Arsenal kimesema kinaendelea na uchunguzi wa jeraha hilo kisha watasema rasmi ni kwa muda gani beki huyo atakuwa nje ya dimba akiuguza jeraha lake.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
Kitengo cha utabibu ya klabu ya Arsenal kimesema kinaendelea na uchunguzi wa jeraha hilo kisha watasema rasmi ni kwa muda gani beki huyo atakuwa nje ya dimba akiuguza jeraha lake.
0 comments:
Post a Comment