Wapili kutoka kushoto ni m/kiti wa CHANETA, Anna Kibira akipoke tiketi za ndege kwa ajili ya wachezaji wa timu ya taifa wa mchezo wa wavu kutoka kwa mkurugenzi wa benki ya Covenant, Mrs. Mwambeja (aliyesimama katikati)

Safari ya timu ya taifa ya mpira wa wavu (netball) ya kuelekea jijini Gaborone nchini Botswana kushiriki mashindano ya Afrika 2015 kwa mchezo wa wavu, sasa imekamilika kwa asilimia kubwa baada ya Covenant bank kugharamia tiketi za wachezaji na benchi la ufundi wa timu hiyo.

Kikosi cha timu ya taifa ya mchezo wa wavu kilichoteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya wavu.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya benki hiyo maeneoya Kijitonyama jijini Dar es salaam,  mwenyekiti wa chama cha netball Tanzania (CHANETA), Anna Kibira, amesema anaishukuru sana benki hiyo kwa kujitokeza kuidhamini timu ya taifa ya netball ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikijiendesha bila ya kuwa na usaidizi wa kueleweka.

"Tunaishukuru benki ya Covenant kwa kuamua kwa moyo mmoja kutoa milioni 40 kwa ajili ya kusaidia safari ya timu ya taifa ya mchezo wa wavu kulekea Gaborone katika mashindano ya Afrika. Tunaahidi kuwa tutaipererusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano hayo kwa kujitahidi kufanya vizuri" Kibira alisema

Aidha, Anna Kibira ameendelea kuwasihi wadau mbalimbali wa michezo nchini kujitokeza kudhamini michezo ya wanawake kwani kundi hilo limesahaulika  kwa muda mrefu, kitendo kinachopelekea kuendelea kukoseka kwa usawa wa mwanaume na mwanamke katika jamii zetu. 


(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top