Baada ya kambi ya siku 20 huko visiwani Pemba, wagosi wa ndima COSTAL  UNION ya jijini 
Tanga sasa leo hii imerudisha majeshi yake nyumbani Tanga tayari kuendelea na ratiba zingine zamwisho kabla ya kivumbi cha ligi kuu Tanzania Bara kuanza pale Septemba 20 mwaka huu.

Displaying ASKARI AKIONGOZA MSFARA WA COASTAL UNION LEO.JPG
Timu ni mashabiki: hao ni baadhi ya mashabiki na wadau wa Costal waliojitokeza leo kuipoke timu hiyo  ikitokea visiwani Zanzibar kwa njia ya ndege. Aliyoko mbele katika ni askari polisi akiongoza msafara huo.


Wapenzi wa COSTAL  UNION walijitokeza kwa wingi wao kulaki timu yao wakati ilipofika katika uwanja wa ndege jijini hapo. Hizi ni picha mbalimbali zinazo onyosha wadau Cost wakipoke timu yao kwa furaha kubwa.

Mechi ya mwisho ya Cost Union ikiwa huko Zanzibar ilishinda kwa idadi ya magoli 10-0 dhidi ya timu iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza.


Displaying AURORA.JPG
Wapili kutoka kushoto ni aliyekuwa mwenyekiti wa Costal Union, Hemed Aurora akiteta jambao na mkuu wa wilaya ya Tanga, mheshimiwa Halima Dendege wakati waki wa mapokezi ya Cost leo hii.
Displaying WACHEZAJI WAKIINGIA KAMBINI.JPG
Baadhi ya wanandinga wa Costal wakielekea kwenye  hostel zao baada ya kushuka kwenye gari iliyowachukua kutoka uwanja wa ndenge.
Leo pia  Septemba 7, 2014 ilikuwa ni siku  maalumu ya klabu ya Costal Union "Costa Union day" ambayo imefanyika katika uwanja wa mabatini huko jijini Tanga.



(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top