Wakati michuano ya kombe la dunia 2014 nchini Brazil ikiendelea kutoa burudani ya kukata na shoka, baadhi ya watu walioko nchini humo kwa sasa akiwemo meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger hawana habari kabisa na burudani hiyo na badala yake wameamua kujiachia katika burudani zingine za ufukweni.
Pichani ni Wenger
Akiwa ni mchambuzi wa mechi za kombe la dunia nchini Brazil katika televisheni ya taifa ya muda ya Ufaransa, Wenger amegeuka kivutio kikubwa sana katika moja ya fukwe maarufu nchini humo wakati akijichanganya na wanafukwe wenzake kwa kucheza beach soka
Wenger ni mpenzi mkubwa beach soka.
Arsene Wenger na klabu yake ya Arsenal alikuwa moto wa kuotea mbali katika ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita baada ya kuwa miongoni mwa timu nne zilizokuwa zinawania ubingwa wa ligi kuu nchini humo lakini baadaye kaishia nafasi ya nne huku akichukua kikombe kimoja cha FA.
0 comments:
Post a Comment