CHELSEA
Thumbnail BOSI wa muda wa klabu ya CHELSEA na kocha wa zamani wa klabu wa LIVERPOOL, RAFA BENITEZ  amesema  anasubiri kwa hamu mchezo wao dhidi  ya LIVERPOOL  utakaopigwa  April 21 mwaka huu dimbani  ANFIELD , huku akisisitiza kuwa undugu kwenye mchezo huo utawekwa pembeni kidogo.
BENITEZ mwenye umri wa miaka 54, anatarajia kutembelea jiji la LIVERPOOL  kwa mara ya kwanza  akiwa na klabu yake  mpya CHELSEA kwa ajli ya michuano ya ligi kuu nchini UINGEREZA inayoendelea kwa sasa baada ya kujiunga na klabu hiyo mnamo mwaka 2010 akitokea Liverpool ambapo alifundisha kwa muda wa mika 6 iliyopita.
Aliendelea kusema kuwa , japo yeye ni mwenyeji wa LIVERPOOL  na familia yake kuishii jijini humo, hilo kamwe halimsumbui na anachotaka ni pointi tatu muhimu ili aendelee kubakia katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu nchini humo.

 
BARCELONA.
Xavi on the cover of BARÇA MagazineMchezaji  wa kati wa vinara wa ligi kuu nchi HISPANAI FC BARCELONA ,  XAVI  ALONSO, mapema leo hii  amesema kuwa hafikiri  kama   mlinda Mlango nambari moja wa Mahasimu wao wa jadi  REALA MADRID ,  IKER CASILLAS,  anaweza kuihama  klabu hiyo na  kujiunge na FC BARCELONA kama mbadala wa  VICTOR  VALDES  msimu ujao wa usajili
XAVI  amesema kuwa, CASILLAS  ambaye amekuwa akisugua  benchi  mara nyingi kwenye klabu ya MADRID, ameelezea hisia zake kwake na kusema kuwa hafurahishwi  na kitendo hicho na muda wowote atakusanya kila kilicho chake tayari kutafuta klabu nyingine ya kuchezea.
Lakini , kwa upande wake  mlinda mlango nambari moja wa  FC  BARCELONA, VALDES  amesema  mkataba wake na klabu hiyo unamalizika  mwakani  na hayuko tayari kuongeza mkakataba  mwingine, hivyo atakuwa huru kuhamia klabu nyingine itakayo muhitaji.
Akiongea na shirika la habari la EL MUNDO DEPORTIVO,  XAVI aliongeza  kuwa yeye binafsi hafurahishwi na kitendo cha CASILLAS kusugua benchi, lakini pia hana imani  kama mlinda lango huyo atajiunga na WAKATALUNYA  msimu ujao wa usajili.


FC  WIGAN
Thumbnail BOSI wa klabu ya WIGAN,  ROBERTO MARTINEZ, kupitia mtandao wa klabu hiyo  amesema walistahili ushindi kwenye mchezo wa jana dhidi ya MANCHESTER CITY, licha ya kutoka vichwa chini baada kuchezea kichapo cha goli 1-0 kwenye mtanange uliopigwa hapo dimbani ETIHAD.

Martinez amesisitiza kuwa  upande wao ulistahili kujiongezea point kwenye mchezo huo kwa kuwa walitengeneza nafasi nyingi za kufunga magoli, lakini wamejikuta wakiwa na wakati mgumu baada ya kupigwa goli moja  na la ushindi  mapema dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza  kupitia  mshambuliaji  matata  CARLOZ TEVEZ.

Lakini pia  klabu ya WIGAN maarufu  kama WANALATIC, licha ya kujihakikishia tiketi ya kucheza  fainalai ya FA na MANCHESTER CITY siku chache zijazo, klabu hiyo inashikilia nafaisi ya 18 katika msimamo wa ligi kuu nchini UINGEREZA ambapo ni miongoni mwa timu  zilizoko kweye  mstari hatari wa kushuka daraja kwenye ligi kuu hiyo.

FRANCIS KIVUYO                             BARAKA MPENJA                           www. Goal .com  4.30 pm
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top