BARCELONA
![]() |
Jordi Roura. |
Kocha msaidizi wa vinara wa ligi kuu
Hispania klabu ya FC BARCELONA maarufu
kama wakatalunya, JORDI ROURA kupitia
mtandao wa klabu hiyo amesema amefurahishwa na kazi nzuri waliyoifanya vijana
wake baada ya kutembeza kipigo kingine cha mabao 3-0 kwa FC. ZARAGOZA
hapo jana.
Wakatalunya ambao kwa sasa wako
kileleni mwa ligi kuu nchini HISPANIA
wakiwa na alama 81 hapo jana
walitembeza kipigo licha ya timu hiyo kukosa majina ya wachezaji wenye majina
makubwa katika ulimwengu wa soka kama vile LIONEL Andrew Jorge MESSI.
ROURA ambaye kikosi chake
kinatarajia kukutana na BAYERN MUUNICH ze bavariani siku chache baadaye kwenye hatua
ya nusu fainali ya klabu bingwa barani ulaya ameendelea kusema kuwa timu
ilicheza vizuri, lakini wachezaji kama
THIAGO SILVA, Alex SONG, pamoja naye TELLO, wameonekana kung’ara zaidi kikosini
hapo.
MANCHESTER CITY.
Mancini. |
Wakati
MANCHESTER CITY ikitembeza kichapo cha
magoli 2-1 dhidi ya CHELSEA, meneja wa klabu hiyo, ROBERTO MANCINI amesema nafasi ya mlinda mlango nambari moja klabuni
hapo JOE HART kwenye fainali ya kombe la
FA itakayo unguruma siku chache zijazo mlinda mlinda mlango namba mbili COSTEL PANTILIMON atasimama golini.
MANCINI amewaambia wanahabari kuwa PANTILIMON
amepata nafasi hiyo ya upendeleo kufuatia kazi nzuri ya kuchomoa mashuti makali
wakati timu yake ikipambana na CHELSEA kwenye mtanange wa kuwania kufuzu hatua
ya fainali ya FC uliopigwa hapo jana uwanja wa WEMBLEY.
![]() |
Adam Maher. |
UHOLANZI.
Mchezaji wa timu ya taifa ya uholanzi
na klabu ya AZ ALKHAMAR, ADAM MAHER, leo
kupitia mtandao wake wa TWTTER amesma
yuko tayari kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu endapo klabu yoyote kubwa itatangaza nia ya
kumsajili.
ADAM mwenye umri wa miaka 19,
amesema miongono mwa klabu ambazo nyota huyo anazitupia jicho ni MANCHESTER
CITY, CHELSEA pamoja na ARSENAL zinazoshiriki ligi kuu soka nchini England.
Vilevile kiungo huyo ameongeza
kuwa, atafurahi zaidi endapo klabu itakayo muhitaji itatoa ofa si ya chini ya URO milioni nane hadi kumi.
Francis Kivuyo Barka Mpenja www.goal.co
0 comments:
Post a Comment