MADRID WATOTA
MAJI DIMBANI SIGNAL IDUNA
PARK.
Wakati FC BARCELONA
wakisikilizia maumivu ya magoli 4-0 kutoka kwa vinara wa ligi kuu nchini
Ujerumani, BAYERN MUNICH, BORUSSIA DORTMUND nayo imeifanya timu ya REAL
MADRID kutoka uwanjani vichwa chini baada ya kuiadhibu timu hiyo magoli 4-1 kwenye mtanange wa kuwania kufuzu
hatua ya fainali ya klabu bingwa barani ulaya uliopigwa hapo jana dimbani SIGNAL IDUNA
PARK.
![]() |
Robert Lewandowski |
Magoli ya BORUSSIA DORTMUND
yalisukumizwa wavuni na mshambuliaji wa
kimataifa, ROBERT LEWANDOWSKI kwa dakika tofauti za mchezo, huku
nyota CRISTIANO RONALDO akifungia timu
yake goli moja na la kufutia jasho mnamo dakika ya 43 ya mchezo ambapo mchezo huo ulifika tamati kwa DORTMUND kuibuka
na ushindi wa magoli 4-1
![]() |
Wachezaji wa Dortmund wakishangilia ushindi. |
Hata hivyo meneja mkuu wa klabu ya BORUSSIA
DORTMUND , HANS-JOACHM WATZKE akiongea
na wanahabari nchini Ujerumani, amesema kwa sasa hawako tayari kumuuza
mshambuliaji ROBERT LEWANDOWSKI kwani
amekuwa ni msaada mkubwa sana klabuni
hapo.
LEWANDOWSKI, mwenye umri wa
miaka 24 amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia kati ya klabu ya BAYERN MUNICH au klabu ya MACHESTER UNITED mwishoni wa msimu huu
MANCHESTER CITY
KOLO TOURE; SIPENDI KUONDOKA
JIJINI LONDON.
Mshambuliaji wa klabu ya
MANCHESTER CITY KOLO TOURE,
kupitia shirika la habari la michezo la SKY SPORT NEWS , amesema anatarajia
kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu lakini amesisitiza kubakia katika
vilabu vya nchini UINGEREZA.
![]() |
Kolo toure |
TOURE mwenye umri wa miaka 32,
alirejea dimbani ETIHAD mwaka 2009, kwa
dau la pound milioni 16 akitokea klabu
ya ARSENAL ambapo amekuwa ni mchezaji muhimu sana klabuni hapo.
Hata hivyo, COLO TOURE ameenda mbali na kusema kuwa anashangaa
ukimya wa klabu yake ya MANCHESTE R CITY
chini ya kocha ROBERTO MANCINI kuhusu kuongezewa mkataba mpya msimu ujao na
amesisitiza kuwa hata kama ataondoka klabuni hapo, matamanio yake makubwa ni
kuchezea vilabu vya nchini UINGERZA kwani anapeanda soka la la nchini
humo lakini pia familia yake inaishi jijini LONDON nchini humo.
FA; LUIS SUAREZ NJE MECHI 10.
Shirikisho la mpira wa miguu nchini UINGEREZA FA,hapo jana limemfungia mshambuliaji wa klabu ya
LIVERPOOL LUIS SUAREZ
kucheza mechi 10 kufuatia kitendo
cha kumng’ata beki wa klabu wa
CHELSEA BRANISLAV IVANOVIC kwenye mchezo wao uliopigwa
dimbani ANFIELD siku chache zilizopita
![]() |
Shuarez katika harakati za kun'gata |
Mchezaji huyo mwenye asili ya nchini URUGUI amenaswa
na kamera za hapo uwanjani aking’nag’aniza meno kwenye mkono wa mchezaji
mwenzake katika kipindi cha pili cha
mchezo ambapo timu zote hizo zilitoka
sare ya kufunguna magoli 2-2
Hivi sasa m shambuliaji LUIS
SUAREZ , analazimika kukosa michezo yote iliyobaki ya kwenye ligi kuu nchini UINGEREZA ikiwa ni pamoja na mchezo wao dhidi ya EVERTON utakayopigwa may 5 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment