CHELSEA
Baada ya klabu ya CHELSEA hapo jana kutwa ubingwa Ligi barani ulaya dhidi ya klabu
ya Benfica, kocha wa muda klabuni hapo Rafael Benitez amesema amefuahishwa sana
na kazi iliyofanywa na vijana wake dimbani
Amsterdam kwani imempa heshima kubwa katika klabu hiyo.
![]() |
Rafael Benitez |
Katika mtanange huo ambao ulikuwa wa
pata shika nguo kuchanika, klabu ya Chelsea ndio ilikuwa ya kwanza kufumania
nyavu ya mwenzake mnamo dakika ya 60 ya chezo, huku mshambuliaji hatari Oscar
Cardozo akisawazishia Benfica goli hilo kwa njia ya penalt mnamo dakika ya 68
lakini baadaye Baranslav Ivanovic akaifungia Chelsea goli la pili na la ushindi
dakia ya 93 ya mchezo huo.
![]() | ||
Fernando Torres akishingilia goli la kwanza |
![]() |
Kushoto ni Torres akikabiliana na Oscar Cardozo. |
Hata hivyo kwa upande wake kocha wa klabu ya Benfika Jorge Jesus akiongea
na waandishi wa habari mara baadayaya kipenga cha mwisho alisema kuwa timu yake
ilikuwa na kila sababu ya kushinda katka mchezo huo kwani timu yake ilicheza
vizuri lakini bahati haikuwa yao.
![]() |
kaazi kwelikweli. |
MANCHESTER UNITED.
Kocha wa mabingwa wapya ligi kuu nchini INGEREZA Manchester United, Sir Alex
Furguson leo kupitia mtandao wa klanu
hiyo amesema anaimani kubwa na kocha mtaraji wa klabu hiyo DAVIDI MOYES
anyefundisha katka klabu ya Evaton kwa sasa.
![]() |
Kushoto, David Moyes na Alex Furguson |
Akiongea kwenye sherehe za mwisho wa msimu klabuni hapo, Furguson
amesisitiza kuwa kocha mtarajiwa klabni hapo anaamini taweza kufanya vizuri
zaidi kwani ni mtu mwenye maadili ya kazi lakini pia ni mtu wa kujituma pale
anapokuwa kazini.
Furguson alikwenda mbali kwa kusema
kuwa kazi aliyoifanya Moyes katika klabu ya Evarton ni kubwa sana kwani ameweza
kuiboresha klabu hiyo kwa muda wa miaka 11 licha ya ukata wa pesa unaoandama
klabu hiyo.
JUVENTUS.
Kocha mkuu
wa klabu ya Juventus AntonioConte, leo
kupita mtandao wa klabu hiyo amedhibitisha kuendelea kukinoa klabu iyo kwa
msimu mwingine uajo baada ya kuwawezesha kuchukua ubingwa wa ligi kuu nchini Italy
maarufu kama seria A.
![]() |
Antonio Conte |
Conte ambaye alinza kuifundisha klabu Juventus tangu mwaka 2011 amesema
ataendelea kukinoa kilabu hiyo kwa misimu mingine ijayo licha kuwepo na tetesi
kuwa klabu ya Real Madrid pamoja na PSG kuonesha nia ya kutaka kumsajili
mwishoni mwa msimu huu.
Lakini pia
rais wa klabu hiyo Andrea Anelli ametilia mkazo kwa usema kuwa Antonio Conte ni mtu muhimu sana katika klabu ya Juventus hivyo msaada wake bado unahitajika kwa kiasi
kikubwa.
0 comments:
Post a Comment