![]() |
Katikati ni Rooney akidondoka wino huku mwenyekiti msaidizi wa klabu hiyo (kushoto) Ed Woodward na David Moyes wakushuhudia . |
Tangu kurejea kwa mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Robin Van Persie kunako klabu ya Man U mwaka 2012 kwa ada ya paundi milioni 22.5 wakati klabu hiyo ikiwa chini ya meneja Alex Ferguson, furaha ya Rooney ilipungua kwa kiasi kikuwa kwa sababu ya kupigwa benji mara kwa mara.
Sababu hiyo ilimfanya nyota huyu kuhisi kama hana sababu ya kuendelea kukipiga katika klabu hiyo na kuanza kuomba kuondoka Oldtraford ili kutafuta klabu nyingine ambayo angepata nafasi ya kucheza mara kwa mara, lakini hiyo ilikuwa tisa kumi ni ile siku klabu ya Man U ilipo mtangaza kocha wa Everton, David Moyes kuwa mridhi wa Furguson baada ya kocha huyo kutanga kubwa manyanga kuendelea kukinoa klabu hiyo mwezi June mwaka jana.
Lakini nyota huyu baada, kimya kirefu juu ya mkataba wake mpya na klabu yake ya Man U, leo amejitia kitanzi mwenyewe cha kuendelea kusukuma gozi klabuni hapo kwa miaka mitano, yaani ataendelea kuwa katika klabu ya Man U hadi 2019, akiwwa anavuna mshahara wa pound 300,000 kwa juma!
![]() |
Rooney akionyesha tabasamu baada ya kusaini kandasi hiyo. |
Mbali na huwa mkataba wa muda mrefu kiasi hicho, Rooney pia amedokezewa kuwa akimaliza kandarasi yake hiyo bado atakuwa na nafasi ya kuwa Balozi wa Man U katika masuala ya kisoka.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment