S
ina shaka kwamba wewe mwana kabumbu mwenzangu unafahamu fika kuwa usiku wa leo March, 11, 2014 ni usiku mwingine wa UEFA champion league hatua ya timu 16 bora ambapo mechi mbili zitapigwa kati ya Bayern Munich dhidi Arsenal katka dimba la Allianz Arena nchini Ujerumani, Huku wao Atletical Madrid wakiwakaribisha AC Millana katika dimba lao la nyumbani Vicent Calderon huko nchini Hispania.

Baada ya Arsenal kushindiliwa magoli mawili kwa sifuri Feb 19, 2014 na bingwa mtetezi wa kombe la klabu bingwa barani Ulaya, Bayern Munich, sasa tayari wako huko jijini Munich tayari kuwakabili wagumu hao kwa mara nyingine tena.

Kulia, Conscienly akijaribu  kumtoka adui wake 

Mbali na Arsenal kuwa na deni kubwa la magoli 2-0 dhidi Bayern usiku wa leo, klabu hiyo pia ina majanga makubwa kwani licha ya Konscienly kuwa miongoni mwa kikosi, bado wanasoka wake wengine  tegemeo wana majeraha mbalimbali hivyo hawatawezi kuitetea timu yao kwa namana yoyote leo.

Hadi Arsenal FC wanapanda pipa jana kuelekea Allianz Arena, walikuwa tayari wameweka wazi kuwa wachezaji wake muhimu; Kieran Gibbs, Jack Wilshere, Nacho Monreal hawatacheza usiku huu dhidi ya vijana wa Pep Guardiola. kwa upandae wake  beki wa kushoto Vermaelen kuna uwezekano wa kucheza kwani hali yake kiafya inaridhisha kiasi.

Akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mchezo wa leo, Arsene Wenger amesema kuwa wanacho amini ni kujituma na kuwa na imani kwa unacho kifanya, pia amesema Bayern wanamtindo wa kushambulia kwa nguvu lakini na wao wamejipanga vizuri na watalinganisha nguvu ya kulinda lango na ya kushambulia ili waibuke na ushindi.

Showing the way: Wenger gets involved in his side's final training session before flying to Munich
Hapana chezea Arsene Wenger wewe!
Kwa upande wake Guardiloa amesema kuna changamoto kubwa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya  msimuhuu kwani timu nyingi zina kiwango kizuri huku akisisitiza kuwa hawazi kutetea ubingwa aliyo nayo kwa sasa bali anacho waza ni kuingia katika hatua nyingine, yaani hatua ya timu 8 bora.    


(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top