Mkaazi mmoja huko nchini China, Kong Huang 35, amegoma kutoka katika gari lake lilipata ajali ya kugongana uso kwa uso na gari lingine akitaka mke wake amdhibitishie kamba ataendelea kuwa naye pamoja na kuwa  amevunjika mguu mmoja katika ajali hiyo.

CEN, China, Truck crash, man refuses to be freed from crash until he speaks to wife, Funny, Weird News, Viral
Kong Huang ndani ya gari kabla ya kupta ajali.
Pamoja na kwamba watu wa huduma ya kwanza walifika kutaka kumsaidia kumtoa ndani ya gari hilo, Huang aligoma kutoka huku akiwasisitiza wangoje kwanza hadi aongee na mke wake juu ya tatizo hilo.

CEN, China, Truck crash, man refuses to be freed from crash until he speaks to wife, Funny, Weird News, Viral
watu wa huduma ya kwanza wakijaribu kumtoa Huang ndani ya gari.
"Lazizi wangu, nina swali moja tu kwako ambalo ni lazima ujibu kwa uaminifu. Nimeumia na bila shaka nitapoteza mguu mmoja" Huang alimwambia mke wake kwa njia ya simu.

Swali langu ni hili; uko tayari kunipenda na kuendelea kuwa na mimi hata kama sitakuwa na mguu mmoja?

Baada ya mke wake kumuahidi kwamba bado ataendelea kumpenda hata kama hatakuwa na mguu mmoja, bwana Kong Huang aliwaruhusu watu wa huduma ya kwanza waendelee kumsaidia.

Chanzo Daily Star.

(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top