Baada ya Manchester United hapo jana Kuonyesha Kiwango kibovu katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya Swancea City dimbani Old Trafford na kulazimishwa kipigo cha magoli 2-1, kocha mkuu wa klabu hiyo Louis van Gaal amemuondoa Luis Nani, Anderson na Wilfried Zaha ili kutoa nafasi kwa wachezaji wapya watakaosajiliwa na klabu hiyo.

United v Swansea Live
Louis Van Gaal.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Vana Gaal amesema kwa anzaia sasa wanandinga hao hawataruhusiwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza, hawataruhusiwa kushiriki chakula na nyota wa klabu hiyo kama vile; Wayne Rooney, Juan Mata pamoja naye Robin Van Persie, wala hawataruhusi kushiriki katika katika vikao na wachezaji wa Man U.
Hamuhitaji tena OT: Pichani ni, Anderson akiwa Nani ambao hawako tena kwenye mipango ya Van Gaal, msimu huu mwengine ni Wilfred Zaha ( hayupo kwenye picha)
Kama hiyo haitoshi inaaminika kuwa, majina ya Luis Nani, Wilfred Zaha, pamoja na Anderso yamesha ondolewa katika makabati ya nguo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo klabuni hapo.

Lakini baada ya hayo yote, Vana Gaal amekitaka kikosi chake cha kwanza  kifike katika uwanja wa mazoezi wa Carington saa kumi jioni kila siku, wakati hao watatu waliotengwa wakilazimika kuja saa kumi na moja kuendelea na mazoezi yao wenyewe.


(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top