Uongozi wa ligi kuu nchini Uingereza umewaonya mashabiki wa ligi hiyo kote dunianiani kuachana na tabia ya kurusha (kupost) video za magoli zisizo rasmi baada ya kitendo hicho kukidhiri katika kipindi cha kombe la dunia 2014 na kusababisha televisheni na makampuni yanayohusika masuala kuonyesha soka kupata hasara.



Kwa kupitia tekinolojia maarufu  iitayo VINE inayomIlikiwa na mtandao wa twitter, mashabiki wanaweza kutuma (kupost) matukio mbalimballi za kisoka zisizokuwa rasmi kwa muda mfupi wakati mechi inaendelea uwanjani. Hadi sasa ukurasa wa VINE (@FootballVines Twitter pages) unakadiriwa kuwa na zaidi ya wadau 539,000 ambao wanaweza kuona video bila malipo ingawaje ubora wa video hizo inaweza kuwa ni ya chini kidogo.

Hata hivyo, uongozi wa ligi ya Uingereza  ambayo itaanza rasmi Juma mosi ya Agost 16, 2014  umesema utafanya jitihada zozote kudhibiti suala hilo msimu huu.

Akizungumza na wana habari mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha EPL, Dan Johnson,  amesema urushaji wa picha za video kwa njia VINE ni kosa, na ni uvunjaji wa sheria za haki za  umiliki.

Dan Johnson, director of communications at the Premier League, warned that posting goal Vines was illegal, as was sharing the videos on websites such as Twitter, and amounted to breaking copyright laws.

"Ni kweli kwamba mashabiki huona kila kitu uwanjani, pia wanaweza kurekodi na kurusha katika mitandao lakini ieleweke kwamba ni kosa na kinyume cha sheria pia. Ni ukiukwaji wa ha haki za umiliki, tunashauri watazamaji/mashabiki waache kufanya hivyo, kwa sasa tunaanda tekinolojia mbalimbali kama vile Crawlers, Vine crawlers pamoja na kuzungumza na uongozi wa Twitter kuonsa ni jinsi gani tutaweza kudhibiti kwa pamoja suala hili. Nafahamu kwamba tutakuwa tumepunguza ladha ya ushabiki kwa mashabiki lakini lazima tuwalinde wale wenye haki za matangazo" Dan John alisema.

Makampumi ya television nao wamelikemea sula la VINE VIDEOS  kwa kiasi kikubwa kwani wanalipa mabilioni ya pesa  ikiwa ni  haki ya kuonyesha soka kwa watazamaji wao. Mfano BT Sports hulipia Uro bilioni 3 kwa msimu  kuonyesha soka kwa watazamaji wake, hivyo wanaona tekinolojia ya Vine ni tishia kubwa katika biashara yao.

source; the guardian.


(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top