Mshambuliajiwa Chelsea Diego Costa, atakuwa nje ya dimba kwa takribani wiki 6 kufuatia kuumia nyama za p aja katika mazoezi ya timu hiyo jana jioni wakati wakijiandaa na mechi ya ligi kuu ya England dhidi ya Everton, jumamosi hii katika dimba la Stamford brigde.
![]() |
Diego Costs ameanza vyema na klabu ya Chelsea kiasi cha kuwa gumza katika ligi kuu ya Uingereza msimu huu. |
Diego Costa aliyejiungana Chelsea julai mwaka huu akitokea mabingwa wa Hispania Athletico Madrid amekwishaifungia chelsea mabao mawili katika mechi mbili za ligi kuu alizocheza msimu huu dhidi ya Burnley na Leichester city.
Kuumiakwa Diego Costa kutamfanya Fernando Torres arudi kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea kuunganana Didier Drogba, hii ni mara baada ya kutojumuishwa katika mechi mbili za mwanzo wamsimu huu.
0 comments:
Post a Comment