Aliyekuwa mkimbiza magari maarufu duniani ya Formula One Langalanga, Michael Schumacher ameruhusiwa kwenda kumalizia sehemu ya matibabu yake nyumbani baada ya kusota kwa muda wa miezi 9 hospitalini kwa sababu ya majeraha ya kichwa aliyoyapata wakati akicheza mchezo kuteleza kwenye milima ya barafu huko nchini Ufaransa mwaka jana
 |
| Schumacher amefanikiwa kuchukuwa ubingwa wa dunia wa F1 mara saba kabla ya kustaafu. |
Kwa mujibu wa meneja wa Schumacher,
Sabine Kehm amesema kwamba pamoja na kwamba utawala wa hospitali ya Lausanne imememruhusu Schumacher, 45 kurudi nyumbani, bado mtaalamu huyo wa LANGALANGA hajapona vizuri na bado anahitaji uangalizi wa hali ya juu.
 |
| Baada ya Schumacher kustaafu kukimbiza magari 2012, akajikita kwenye mchezo mwingine wa kuteleza kwenye milima ya barafu. Hata kaa asahau tarehe ya Desmba 29, 2013 baada ya kupinduka wakati akionyesha makeke katika mchezo huu huko nchini Ufaransa na kupata jeraha la kichwa. |
Michael Schumacher mwenye asili ya nchini Ujerumani alistaafu kushiriki mashindano ya kukimbiza magari mwaka 2012 akiwa amedumu katika mchezo huo kwa muda wa miaka 19 , ni mmoja wa watu wengi waliofanikiwa kufanya vizuri sana katika mchezo huo.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment