Rio Ferdinand.
Baada ya uchunguzi kukamilika shirikisho la kandanda nchini Uingereza FA, limemfungia beki wa Queens Park Rangers, Rio Ferdinand  mechi tatu na faini ya pauni 25,000 kwa kosa la kuandika ujumbe wa matusi katika mtandao wake wa twitter mwezi uliopita

Inadaiwa Ferdinand 35 alitumia neno 'SKET' katika moja ya jumbe zake kwenye mtandao wake wa twitter mwezi Septemba 2014 wakati akijibizana na baadhi ya watu waliokuwa wakihoji msaada wake katika klabu ya QPR.



"SKET , ni neo lisilokuwa rasmi la kimarekani linaloaminika kuwa ni la kimadharau/kiubaguzi wa kijinsia  (wanawake) " FA ilisema.

Matusi na aina yoyote ya ubaguzi ni miongoni mwa mambo yanayopingwa sana katika tasnia ya mpira wa miguu.

(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top