Na Frank Mgunga Momanyi, Dar es salaam.[Makala]
Wakati timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ikitarajiwa kushuka ugani hapo kesho katika mtanange wa kukata na shoka dhidi ya timu ya taifa ya benin mchezo utakaopigwa katika dimba la uwanja wa taifa jijini dare s salaam, baadhi ya wadau wa soka nchini wamesema wanaimani na Taifa Stars na kuamini kuwa wataipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mchezo wa hapo kesho.

Akizungumza na mishemishezamtaa blog, mchezaji wa zamani wa klabu ya yanga sekilojo chambua amesema mchezo wa hapo kesho ni kiwango sahihi kwa stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro premium lager chini ya kocha mholanzi mart nooij ambaye anapenda kutumia mfumo wa 4:3:3 lakini je mfumo huo utaweza kuizamisha benin hapo kesho?
Chambua alisema mfumo wa kocha sio kigezo cha kuifanya timu yoyote kuweza kuibuka na ushindi bali juhudi binafsi za wachezaji ndicho kinaweza kuipa ushindi timu yoyote ile duniani.
"Mfumo wa kocha siyo kigezo cha kuifanya timu yoyote kuweza kuibuka na ushindi bali juhudi binafsi za wachezaji na ushirikiano ndicho ninaweza kunaweza kuipa ushindi timu yoyote ile duniani, hivyo wachezaji wanatakiwa kujituma hapo kesho ili kuhakikisha wanaipa ushindi taifa stars na kuweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania”
Lakini pia kwa upande mwingine Chambua alisema wingi wa mashabiki wa mchezo wa soka katika mchezo wa kesho itakuwa ni chachu kubwa kwa timu ya taifa ya Tanzania kuweza kuibuka na ushindi.
Stars ambayo inashuka dimbani ikikumbuka kipigo kutoka kwa timu ya taifa ya Msumbiji na kuweza kuondolewa katika mitanange ya kufuzu michuano ya kombe la mataifa barani afrika, hapo kesho itashuka ugani ikiwategemea wachezaji wake mahiri wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi kama vile Mbwana Ali Samatta, Thomas Ulimwengu, Mwinyi Kazimoto pamoja na Juma Luizio anayekipiga katika klabu ya Zesco fc ya nchini Zambia.
0 comments:
Post a Comment