Kihistoria, kesho siku ya Jumapili, Aprili 12, 2015, ni 'derby' ya 169 kati ya Manchester United dhidi ya Manchester City katika michuano ya ligi kuu nchini Uingereza msimu wa 2014/2015. Ni wazi kwamba mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na uzuri wa timu zenyewe na nafasi zilizopo katika msimamo wa Baclays Premier League. Mashetani wekundu wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 62, alama moja juu ya mahasimu wao Man City ambao wamejikita katika nafasi ya nne wakiwa wamejikusanyia alama 61 mpaka sasa.
Licha ya kwamba Man City ndiyo inayoshikikilia reokodi ya kumpiga Man U magoli mengi zaidi hivi karibuni (2011/2012: Man U 1-6 Man City), bado mashetani wekundu wanaonekana kupewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa kesho kulingana na matokeo aliyoyapata katika mechi za hivi karibuni.
Katika mechi tano za ligi kuu za hivi karibuni alizocheza Man U, amefanikiwa kushinda mechi nne, wakati mahasimu wao Man City wao wamejikuta wakishinda mechi mbili tu kati ya tano walizocheza. Hii ni ishara kwamba Mashetani wekundu wapo katika kiwango cha hali ya juu ukilinganisha na Man City kuelekea katika mchezo wa kesho ambao utapigwa dimbani Oldtrafford.
Lakini ukiachilia mbali rekodi na sababu zilizotajwa hapo juu, mchezo wa kesho utategemea zaidi jinsi makocha wa timu zote mbili; Louis Van Gaal-Mn U pamoja na Manuael Pellegrini-Man City watakavyo kuwa makini katika kuteua na kupanga vikosi vyao, hii ni kwa sababu timu zote mbili zinaonekana kukamilika kila idara.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment