Wachezaji wa Gor Mahia walikuwa wepesi sana kutafuta mpira (kukaba) mara unapokuwa kwa maadui, pia  wakipata mpira wanapiga pasi za kushtukiza
Kadi hiyo itammfanya Ngoma kukosa mechi ijayo, alikuwa mwiba mkali sana kwa idara ya ulizi ya Gor Mahia 
Jinanamizi la kupoteza mechi ya kwanza katika mashindano ya CECAFA KAGAME CUP limeendelea kuwaandama wanajangwani baada ya klabu yao leo kukubali kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya vinara wa ligi kuu nchini Kenya, Gor Mahia FC katika mechi ya umfunguzi wa mashindano hayo kwa msimu wa 2015 ambao ulifanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kufumania nyavu ya Mahia mnamo dakika ya 9 ya mchezo huo baada ya beki wa Gor Mahia  kujifunga, goli ambalo liliwachukuwa Wakenya  dakika 13 kulirudisha na baadaye kuongeza goli la pili na la ushindi katika dakika za lala salama.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kipute hicho, kocha wa Yanga SC, Van Der Pluijm alisema matokeo ya 2-1 sio ya kusikitisha sana ingawaje walipaswa kushinda mchezo huo.
“Tumecheza mchezo mzuri sana lakini Gor Mahia walituzidi kidogo na ndiyo maana mechi imemalizika kwa Gor Mahia kuibuka na ushindi wa magoli 2-1. Mapungufu makubwa niliyo yaona kwa  wachezaji wangu wengi ni  kushindwa kushindana na wapinzani kwa nguvu za mwili na ndiyo maana wachezaji wangu walikuwa wakidondoshwa mara kwa mara uwanjani” Alisema Pluijm.
Aidha, Pluijm aliwahakikishishia wana habari kwamba mapungufu yaliyotokea katika mechi ya leo yatarekebishwa haraka sana na hatimaye kupata ushindi katika mechi zijazo.
Kwa upande wake Kocha wa Gor Mahia, Frank Nuttal, alisema anamshukuru Mungu kwa timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya wenyeji Yanga Sc klabu.
“Kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya klabu kubwa Afrika Mashariki na kati, Yanga SC ni kitu cha kujivunia sana. Tunaamini ushindi huu utatupatia nguvu ya kupambana zaidi katika mechi zijazo”. Alisema Nuttal.
Lakini mbali na hayo; mfungaji wa goli la Yanga, Donald Ngoma  atalazimika kukose mechi moja ijayo baada ya kutolewa nje na mwamuzi mnamo dakika ya 32 ya kipindi cha kwanza kwa utovu wa nidhama baada ya kuenekana kumpiga kofi mchezaji wa Gor Mahia akidai alimchezea rafu.
Katika historia ya mashindano haya, Yanga SC  imepoteza mechi ya kwanza mara tano lakini ikiwa imechukuwa ubingwa wa mashindano haya mara nne.



(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

0 comments:

Post a Comment

 
Top