AMA KEWELI BIASHARA NI MATANGAZO.

Siku hizi ukipita mitaa ya miji mbalimbali humu nchini,utaona mabango mbalimbali yanayonadi biashara tofautitofauti.

Miongoni mwa matangazo yanaoshika kasi siku hizi ni pamoja na yale yanayotangaza waganga wa jadi wenye uwezo wa kuboresha mapenzi, kurudisha mali zilizoibwa, na mengine mengi kama vile wa  kusafisha nyota.

Katika pita pita zangu kwenye mtaa mmoja jiji la Dar es salaam nimeona tangazo linalomnadi mtu mwenye uwezo wa kuwaunganisha watu na Freemasoon kama inavyoonyeshwa na tangazo hapo juu ambalo limeniacha na maswali mengi sana!

Nimekuwa nikijiuliza kwamba  hawa watu wao wametoa wapi huo uwezo? ....wanaleseni ya hizo kazi?..kwanini hawapendi kusema sehemu ofisi zao zilipo zaidi ya kutoa namba za simu tu?

Lakini ikumbukwe jinsi watu hawa wanaopenda kujitambulisha kwa jina la madaktari wajadi walivyoweza kusababisha machafuko ya amani nchini miaka michache iliyopita, Watu wengi wakiwemo wale wenye ulemavu wa ngozi (alibino) wamekuwa wakiuwawa na sehemu ya viungo vyao vya mwili kuchukuliwa eti kwa sababu ya kwenda kutumia katika harakati za kutafuta pesa, na haya yote yamesababishwa na hawa waganga feki. hii inasikitisha sana!

Napenda kutoa ushauri kwa watanzania  wenzangu wanaojihusisha ama wanaofikiria kujihusisha na shughuli za kishirikina ikiwemo  hiyo ya Freemasoon waachane nazo mara moja kwa kuwa hazina ukweli wala uhalisiwa wowote kwa kiasi kikubwa zaidi ni kuchanganyana akili tu na mwisho wa siku kuishia katika shimo la hewa. Lakini vilevile serikali ina mkono mrefu sana kiasi kwamba inaweza kupiga marufuku mambo haya na hatimaye kutoweka kabisa.

Maswli;
1.Unafahamu watu wanaojishughulisha na Freemasoon?
2.Unawafahamu waliofanikiwa kupiti Freemasoon?
3.Nini mtazamo au maoni yako juu ya hili? (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top