Bunge kubadili ratiba yake.
Bunge
la bajeti ambalo huanza shughuli zake mwezi Juni hadi Agosti,
linatarajia kubadili ratiba yake kwa kuanza Aprili na kumalizika Juni
30.
Lengo la mabadiliko hayo ni kulinda sheria ambayo inataka fedha za serikali zinazopitishwa na Bunge zianze kutumika Julai Mosi.
Ofisa habari wa Bunge, Prosper Minja, alisema kwa sasa kamati ya uongozi bado inajadiliana ili kuona kama suala hilo linawezekana.
“Bado kamati ya uongozi ambayo inapanga shughuli za Bunge inajadiliana ili kuona kama suala hilo linawezekana na kama itakubaliana, Bunge la bajeti litakuwa linaanza shughuli zake Aprili na kumalizika Juni 30,” alisema Minja alipokuwa akizungumza na NIPASHE.
Alisema mabadiliko hayo yanafuatia kufanyiwa kazi ushauri lilitolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kwa mujibu wa Minja, CAG alishauri fedha zinazopitishwa katika bajeti zianze kutumika siku ambayo Waziri Mkuu anatoa hotuba ya kuahirisha Bunge na kazi ambayo huifanya Agosti.
Alifafanua kuwa siku ambayo Waziri Mkuu anatoa hoja ya kuahirisha Bunge, fedha zinakuwa zimeanza kutumika tangu Julai Mosi, na kwamba huko ni kukiuka sheria.
Minja alisema ikiwa vikao vya bajeti vitahitimishwa Juni 30, sheria itakuwa inazingatiwa kwa kuwa serikali itaanza kutumia fedha zilizopitishwa na Bunge kuanzia Julai Mosi.
Alisema ikiwa Kamati ya Uongozi itakubaliana, Bunge linaweza kuwa linakutana mara tatu kwa mwaka badala ya mara nne.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment