Unapozungumzia mapinduzi ya kiuchumi nchini hauna budi kuipa kilimo nafasi ya kwanza, hii ni kutokana na ukweli kwamba shughuli zingine za kiuchumi kama vile viwanda pia vinategemea kilimo ilikupata malighafi.Mfano viwanda vya nguo hutegemea kilimo cha pamba.

Tatizo linalokabili nchi nyingi za kiafrika kiuchumi, Tanzania ikiwa mojawapo ni mipango mibovu ambayo inawekwa na viongozi walioko madarakani. Mfano wakati wa azimio la Arusha 1965 Baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere aliamuru masomo  ya kilimo mashuleni kuwa ya lazima...lakini baadae mitaala ilibadillishwa na kwa bahati mbaya somo la kilimo likawa siyo la lazima.

Sasa ukijaribu kuangalia hapo unagundua kabisa kuwa Watanzania hatujiulizi na wala  hatuna uhakika na mipango yetu, shule ndiyo sehemu ambapo unaweza kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi. Hivyo kama kweli tunataka kufanya mapinduzi ktk kilimo sharti tuipe somo la kilimo nafasi kubwa mashuleni kuanzia shule za msingi, sekondari hadi vyuo vikuu.

Ni aibu kubwa sana kwa nchi ya Tanzania yenye ardhi nzuri  yenye rutuba kulia njaa ya chakula kila siku, lakini pia napenda kuipongeza serikali  kwa jitihada ambazo imekuwa ikifanya ili kuboresha hali ya kilimo nchini kupitia kampeni zake za KILIMO KWANZA... inajaribu lakini bado sana kwa kuwa kilimo 'kwanza' bila elimu ya kilimo cha KISASA ni ndoto!


(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

0 comments:

Post a Comment

 
Top