MANCHESTER CITY.
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester city
Thumbnail
Niall Quinn.
NIALL QUINN,  mwenye uri wa miaka 46 leo kupitia mtandao wake wa TWITER amesema kwamba kukosekana kwa wachezaji kama EDEN HAZARD na ROBIN VAN  PERSIE  ambao city ilishindwa kuwasajili kumesababisha klabu hiyo kucheze kwa taabu, hivyo viongozi wasirudiemakosa kama hayo.
QUINN ameongeza kuwa licha ya Man City kupata pointi 3 kwa  kuwafunga watani wao wa jadi mabao 2-1 katika uwanja wa Old Traford, ni lazima klabu hiyo ifanye usajili makini msimu ujao kama inahitaji kuingia soka la ushindani zaidi.
Katika mchezo wa jana ligi kuu soka nchini Uingereza bao la kwanza la city lilifungwa na nyota wake James Milner, huku la pili likitiwa kambani na Sergio Kun Aguero akitoke benchi.
Bao pekeee kwa United waliokuwa mbele ya umati wa mashabiki wake lilifungwa na beki PhIL Jones.


  PSG.

Thumbnail
Thiago Silva.
Beki wa klabu ya PARIS SAINT GERMAIN ya  UFARANSA, THIAGO SILVER,  amewaambia wanahabari wa nchini humo kuwa,  kwa sasa yuko tayari kuhamia klabu ya  FC BARCELONA msimu ujao endapo klabu hiyo itaonyesha tena  nia ya kutaka kumsajili baada ya kushindwa kufanikiwa  msimu uliopita.

SILVER  RAIA wa BRAZILI  alisajiliwa na klabu ya PSG mapema msimu uliopita baada ya FC BARCELONA kushindwa kuchangamkia dili hilo.

Lakini kwa mara nyingine tena  FC BARCELONA maarufu kama WAKATA LUNYA   wamekuwa wakihusishwa na tetesi za kutaka   kumsajili mwanasoka kutokana na kiwango kizuri alichoonesha katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya kati ya PSG na Barca na mtanange huo kumalizika kwa sare ya 2-2.


CHELSEA
                         
Thumbnail
Frank James Lampard
Wakala wa kiungo wa Chelsea  FRANK  JAMES  LAMPARD ,  STEVE KUTNER,  kupitia mtandao wa kijamii wa Goal.com  mapema leo amesema kuwa,  kutoshiriki kwa LAMPARD  kwenye  zoezi la upigaji wa picha ya matangazo na wachezaji wenzake, haina madhara yeyote kwa mchezaji huyo siku za usoni.
Kiungo huyo ambaye mkataba wake na klabu ya CHELSEA unaisha mwishoni mwa msimu huu, hakushiriki kwenye upigaji wa picha za Frank James Lampard.matangazo ya  ADIDAS KIT  kwa madai kuwa  picha hizo hazina umuhimu wowote.
KUTNER  ameendelea kusema kuwa kamekuwepo na taarifa za zoezi hilo ambapo wachezaji  kama  FERNANDO TORRES na JUAN MATA  wameonekana wakipiga picha, lakini Lampad ameshindwa kuhudhuria kutokana na majukumu ya kifamilia.
 LAMPARD mwenye umri wa miaka 34  amekuwa  akihusishwa na tetesi za kujiunga na vilabu kama vile; LA GALAXY , PARIS SAINT GERMAIN  na JUVENTUS  kabla  ya  CHELSEA kumuongezea mkataba wake unaoisha mwishoni mwa msimu huu.

Kivuyo Francis           Baraka Mpenja               www.goal.com
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top