Nguli wa mchezo wa soka wa nchinini Ufaransa Zinedine Zidane amekataa ushauri wa rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez ya kuridhi mikoba ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Jose morinho aliyekimbilia kunako klabu ya Chelsea huku akisisitiza kuwa uzoefu wake bado ni mdogo sana kuifundisha klabu ya Real Madrid.
![]() |
Zinedine Zidane 'Zizu' |
Hata hivyo Perez, ambaye amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa rais wa Madrid kwa miaka mingine minne ijayo, ameendelea kusisitiza kuwa bado matarajio yao makubwa yako kwa kocha wa PSG, Carlo Ancelote na wanafanya kila jitihada kuhakikisha wamsainisha kocha huyo.
Kocha wa klabu ya Beyern Munich Jupp Heynckles aliyetangaza kustaafu kukinoa
klabu hiyo baada ya kuiwezesha kunyakua kombe la EUROPA champion legue msimu
uliopita, amekanusha tetesi zinazodai kuwa huenda akajiunga na klabu Real Madrid
mapema msimu huu
![]() |
Jupp Heynkles katikati akinyanyua kombe walilolitwa dhidi ya Borussia Dortmund kwenye fainali ya Europa Champion League 2012/2013 |
Akiwa ni miongoni mwa makocha wanaopewa
kipaumbele ya kuridhi mikoba ya
aliyekuwa kocha wa Real Madrid Jose Morinho, mzee Hynckles mwenye umri wa miaka
68 amesema kwa sasa hana mpango wa kujiunga na klabu yoyote na badala yake anajipumzisha kidogo huku nafasi yake
ikichukuliwa na aliyekuwa kocha wa wa Barcelona, Pep Gardiola.
Lakini kwa upande wake
mwenyekiti wa klabu ya Bayern Karl-Heinz
Rummenigge, amesema licha ya Heynckes kutangaza
kustaafu kufundisha kandanda, bado
milango iko wazi kwa kocha huyo endapo atahitaji kurudi kukinoa klabu hiyo kwa
siku zingine zijazo.
0 comments:
Post a Comment