![]() |
Robert Lewandowski |
Hivi karibuni Lewandowski
amekaririwa akisema huenda akajiunga na mabingwa wa EUROPA CHAMPIONS LEAGUE, Buyern Munich
mwishoni mwa msimu huu kitendo ambacho kimefanya klabu mbalimbali kama vile Barcelona, Arsenal, Chelsea na Manchester United kutafuta kila mbinu ya
kumsajili
Lewandowski ameongeza kuwa kwa sasa hakuna klabu inayoweza kumshawishi kwa kiasi chochote cha pesa kwani kwa sasa ameota mizizi ya kutosha katika klabu ya Dortmond.
Hata hivyo Lewandowski ameendela kuwa katika kiwango kizuri cha soka kama ilivyokuwa mwaka jana na kwa sasa amekwisha ifungia timu yake magoli 13 katika michezo 17 alizocheza
Lewandowski ameongeza kuwa kwa sasa hakuna klabu inayoweza kumshawishi kwa kiasi chochote cha pesa kwani kwa sasa ameota mizizi ya kutosha katika klabu ya Dortmond.
Hata hivyo Lewandowski ameendela kuwa katika kiwango kizuri cha soka kama ilivyokuwa mwaka jana na kwa sasa amekwisha ifungia timu yake magoli 13 katika michezo 17 alizocheza
Naye Mshambuliaji wa Chelsea, Andrew
Schurrle amesema malalamiko ya meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho juu ya kipigo
cha magoli mawili walichokipokea kutoka kwa NEWCASTLE siku chache zilizopita, imeeleweka
na hali hiyo imewafanya wajipange vyema kuelekea mchezo wao dhidi ya Schalke 04
utakaochezwa leo hii.

Andrew Schurrle
Akiongea na waandishi wa
habari leo hii, Shurrle amesema kuwa ni wazi meneja Jose Mourinho
hakufurahishwa kabisa na kiwango walichokionyesha dhidi ya Newcastle hivyo wao
kama wachezaji hawana namna ya kukwepa lawama
Andrew Schurrle
Aidha Shurrle ameendelea kusisitiza kuwa timu ya Schalke 04 ni miongoni mwa timu ngumu hivyo hawana sabubu ya kuibeza kwa namna yeyote kwani timu hiyo pia inawachezaji wazuri kama vile Julian Draxler, Kevin-Prince Boateng and Adam Szalai ambao wanaweza kuleta upinzani wa hali ya juu katika mechi hiyo
Tukiachana na habari hizo pia, Meneja wa klabu ya Manchester City, Manuel Pelegrini amesema amegadhabishwa sana na maumivu ya msuli uliompata mshambuliaji wake David Silva wakati timu yake ikikabiliana na timu CSKA Moscow hapo jana ambapo timu ya Man City iliweza kuibuka na ushindi wa magoli 5-2

Pia David Silva amelazimika kuhairisha ziara ya matembezi na timu yake iliyofanyika leo huko London katika kituo kimoja kinachojulikana kama ExCeL na badala yake ameenda hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Chanzo: Goal.com
0 comments:
Post a Comment