Hatimaye mshambuliaji wa klabu ya wabeba mitutu wa London Arsenal fc, Theo James Walcott amedhibitika kuwa nje ya dimba kwa muda usiopungua miezi sita kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata hapo jana wakati wa mechi dhidi ya mahasimu wao Tottenham, mchezo ambao ulifika tamati kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 0
 |
T.Walcott akitolewa nje baada ya kuumia goti. |
Walcott aliyekipiga katika klabu ya Southampton kabla ya kujiunga na Arsenal mwaka 2006 kwa ada ya Uro milioni 5, kwa sasa analazimika kufanyiwa upasuaji wa goti ili kuweza kubaini tatizo, kitendo kitakacho mlazimu kukosa michezo yote iliyobaki ya ligi kuu ya nchini Uingereza pamoja na michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kuanza kurindima hivi karibuni huko nchini Brazil.
Walcott amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 21 kwenye EPL pamoja na timu yake ya taifa na amefanikiwa kufikisha jumla ya magoli saba kwa michezo yote.
 |
T.Wallcot akionyesha ishara iliyotaka kumgarimu |
Hata hivyo shirikisho la mpira wa miguu la nchini UingerezaFC limesema T.Walcott hatapata adhabu yoyote kwa sababu ya kuonyesha ishara ya vidole viwili kuelekea kwa mashabiki wa Tottenham wakati akitolewa nje ya uwanja baada ya kuumia kwani imedhibitika kuwa ishara hiyo haikuwa na nia mbaya bali alikuwa akimaansha ushindi wa magoli mawili.
Chanzo; Goal.com
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment