Kama kawaida klabu ya Young Africans na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara imeendelea kujifua katika viwanja mbalimbali hapa jijini Dar es salaam, ambapo leo kikosi chote kilikuwepo katika uwanja wa Tanganyika Packers mitaa ya Kawe kwa ajili ya mazoezi.
Pichani ni klabu ya Young Africa wakiomba duwa kabla ya kuanza mazoezi |
mazoezi hayo ni sehemu ya mpango kabambe wa kujifua kuelekea duru la pili la michuano ya ligi ya VODACOM inayotarajia kuendelea kurindima katika viwanja mbalimbali hapa nchini siku chache zijazo.
Anaye onekana katikati (bukta nyeusi) ni kocha wa muda wa Yanga, Bonifas Mkwasa akisimamia mazoezi. |
Kuanzia upande wa kushoto mwa picha hii ni Juma Kaseja, Barrthes/Ally Mustapha na Dida wakipokea maelekezo kutoka kwa kocha wao Juma Pondamali. |
*Picha na Yusufu Nuru*
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment