Mtanange kati Villarreal na Celta Vigo uliokuwa  unachezwa hapo jana usiku dimbani El Madrigal ulisimamishwa kwa muda wa nusu saa baada ya mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni shabiki   kutupa bomu la machozi kwenye goli la Villarreal.


In the smoke: Villarreal's Jonathan Pereira runs to kick a tear gas canister during the match with Celta Vigo at El Madrigal
Kushoto ni mchezaji wa Villareal, Jonathan Pereira akijaribu kuondoa nje ya uwanja chupa hiyo yenye gesi kwa kupiga teke. 
Tukio hilo lilitoke dakika saba tu kabla ya kipenga cha mwisho kupulizwa na kusababisha taharuki kubwa kwa watu wote waliokuwa uwanjani pale kwani bomu hilo lilitoa moshi mkubwa wenye kuwasha pua na macho kama lile linalotumiwa na polisi.

Taking their leave: Fans leave El Madrigal after a canister of tear gas was thrown on to the pitch
 Mashabiki wakikimbia nje ya uwanja kwa sababu ya moshi mkali
Mchezo huo uliendelea tena baada ya kusimamishwa kwa nusu saa, ambapo Celta Vigo waliweza kuongeza goli la pili mmona dakika ya 90 kupitia mshambuliaji Nolito, goli la kwanza la Vigo lilipatikana dakika ya 83 kupitia mshambuliaji Fabian Orellana.

Magoli hayo mawili ya Celta Vigo dhidi ya Villarreal inaifanya Vigo kuwa katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Hispania ikiwa na pointi  29 huku Villareal wao wakiwa katika nafasi ya tano wakiwa na pointi 40 kibindoni

Credits; Daily mail (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top