Kwa mujibu wa website ya Olando Pirates, wamesema wameamua
kumchukua Vermezovic baada wa kocha wao
Roger de Sa kujiuzulu kuendelea kukinoa klabu hiyo siku chache zilizopita huku
wakisisitiza kuwa Vladimir Vermezovic ndiye
chaguo lao sahihi kwa sasa.
![]() |
Vladimir Vermezovic |
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo hii mmiliki wa
klabu ya Olando Pirates Irvin Khoza kwa
upande wake amesema hana wasiwasi na kocha
Vladimir Vemezovic kwani analifahamu soka la Afrika Kusini kwa
muda mrefu na kwa sababu hiyo anamkaribisha kwa mikono miwili.
Kama kawaida yake meneja wa klabu ya Chelsea ama ukipenda
unaweza kuwaita FARASI MDOGO , bwana
Jose Mourinho mapema leo hii amesema
kuwa Aarsenal kwa sasa hawawezi kutumia kisingizo cha umri mdogo wa wachezaji
wake katika ligi kuu ya uingereza kwani
msimu huu wachezaji wake wote ni wakubwa.

Mourinho alikwenda mbali
zaidi na kusema kuwa Arsenal amabo wako nyuma yao kwa point moja katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza
ni timu nzuri sana msimu huu kwani ukiachilia mbali sababu ya kuwepo kwa
wachezaji wengi wenye miaka zaidi ya mitano klabuni hapo, Pia Arsenal
imefanikiwa kuwasajili wachezaji wazuri sana katika klabu yao msimu huu mfano Mezuit
Ozil, Santi Carzola pamoja naye Per Mertasacker.
USA
Timu ya
taifa ya Marekani kupitia mtandao wao leo wamedhibitisha kupokea timu ya taifa
ya Mexico, Aprili mbili mwaka huu kwa ajili mechi ya kujipima nguvu ikiwa ni
sehemu maandali yao ya kuelekea kwenye michuano kombe la dunia
litakalo anza kutimua vumbi Juni mwaka huu chini Brazili.
Akizungumza na vyombo
mbalimbali vya habari kocha wa timu ya taifa ya Marekani Jurgen Klinsmann amesema wanatarajia kutumia mchezo huo ambao
utachezwa katika jiji la Arizona kutengeneza kikosi kitakacho kwenda kupeperusha
bendara ya taila la Marekani huko nchini
Brazili
Mchezo wa kirafiki wa
hivi karibuni kuwa kuchezwa na timu hizi ulikuwa ni Augusti 15, mwaka 2012
ambapo Marekani waliweza kutumia vyema uwanja
wa nyumbani na kuifunga Mexico goli moja kwa sifuri.
Credits: mtandao
0 comments:
Post a Comment