Baada ya mzozo uliodumu kwa muda mrefu sasa,klabu ya Westbromwich Albion imeamua kumtupia virago mshambuliaji wao, Nicolas Anelka kwa sababu ya ishara yenye utata (Quenelle gesture) aliyo ionyesha baada ya kufunga bao wakati timu yake ikicheza dhidi ya West Ham United mwezi December.

Kilicho mfanya Anelka kulimwa kalamu nyekundu na West Brom ni kauli aliyo itoa jana (14-03-2014) katika mitandao ya kijamii ambayo inadaiwa kuwa amesema hayuko tayari kuendelea kukipiga kunako klabuni hapo kwa sababu ya masharti magumu aliyopewa na klabu hiyo.

Kulia ni Nicolas Anelka akionyesha ishara ya quenelle
''kutokana na mazungumza kati yangu na maafisa wa klabu, kuna masharti kadhaa wamenipa  kabla ya kujiunga tena na klabu hiyo, masharti amabyo siwezi kuyakubali''. Anelka aliandika hivyo.

Mara baada ya Anelka kuonyesha ishara hiyo ambayo inadaiwa kuwa ya kibaguzi wa rangi dhidi ya Wayahudi iliyokuwa inatumiwa na jeshi la chama cha NAZI , shirikisho la mpira wa miguu nchini Uingereza (FA) ilimpiga nyota huyo faini ya pauni 80000 na kumsimamisha kucheza michezo mitano.

Hata hivyo, WestBrom, wamesemakuwa masharti walioyompa Anelka ni pamoja na kumtaka awaombe radhi mashabiki, wadhamini wa klabu hiyo na wanajamii kwa ujumla kwa sababu ya adhara iliyotokana na ishara yake aliyo ionyesha December 28 na pia akubali kutozwa faini.




(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top