Na Francis Kivuyo, Dar es salaam.
Miongoni mwa njia kuu ya mapato kwa nchi nyingi duniani ni
kodi. Kodi ni kiwango fulani cha malipo (ada) ambayo serikali ya nchi fulani huwatoza
watu wake kupitia shughuli wanazozifinya, mishahara wanayolipwa kutokana na kazi wanazozifanya au kupitia
huduma wanazopokea.
Kwa bahati mbaya licha ya kodi kuwa na umuhimu mkubwa katika
ukuzaji wa uchumi katika nchi fulani, watu wengi hawapendi kulipa, siyo
masikini wala tajiri na ndiyo maana ukizungumzia suala la kodi watu wengi
watakumbia kabisa!
March 13 2014 ilikuwa ni siku ya majonzi makubwa kwa aliyekuwa raisi wa klabu ya Bayern Munich,
Bw. Uli Houness baada ya mahakama kuu ya nchini Ujerumani kuamuru afungwe jela
kwa muda wa miaka mitatu na nusu baada ya kukutwa na kosa la kukwepa kulipa
kodi.
![]() |
Uli Houness. |
Houness mwenye umri wa miaka 62 anatuhumiwa na serikali ya
Ujerumani kwa kosa la kuficha baadhi ya hela zake katika moja ya benki huko
nchini Uswiss ili kukwepa kulipa kodi inayotokana na kipato chake ( lipa kadiri
uingizapo), ambapo baada ya uchunguzi wa kina kufanyika aligundulika kuikosesha
serikali yake kati Uro milioni 3.5 hadi Uro milioni 7 kutokana na hela hizo alizo
zificha.
Kumbuka Uli Honess ni miongoni mwa watu walio onyesha
mchango mkuwa sana katika soka la Ujerumani, kwani amefanikiwa kuiwakilisha
nchi yake katika michuano ya kombe la dunia mwaka 1986 akiwa mshambuliaji mzuri
tu wa timu ya taifa mbali na kuiacha klabu yake ya Bayern ikiwa ya kwanza nchini
ujerumani kwa kuwa na uchumi mzuri, lakini pamoja na hayo yote serikali yake
haikupepesa macho hata kidogo juu ya kosa lake.
Lengo langu kuandika makala hii ni kuonyesha utofauti ulipo
kati ya uwajibakaji wa serikali za nchi za wenzetu na ya kwetu ( Tanzania)
katika suala zima la ukusanya wa kodi ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha mapato
humu nchini.
Mara kwa mara tumekuwa tukisikia minong’ono kibao kuhusu wanasiasa wengi na wafanya biashara wa
Tanzania wanaosadikiwa kuficha hela zao katika
benki zilizopo nchi za nje, mojawapo ikiwa ni nchi ya Uswiss ambayo ndiyo
inatajwa kuwa chaka maarufu kwa kuhifadhia hela na rasirimali kutoka nchi
zingine, lakini cha ajabu watu hawa hawatajwi wazi wazi wala hawashitakiwi!
Mwishoni mwa mwaka jana mheshimiwa Zitto Kabwe na mbunge wa
Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA kupitia vyombo mbalimbali vya habari alitanganza
kuwa anawafahamu wanasiasa na vigogo wa Tanzania walioficha pesa zao kwa siri
katika benki za nchini Uswissi lakini baadaye alishindwa kuwataja kwa majina, lazima
kuna kitu nyuma ya sinema hii.
Mbali na sula la kuficha hela nje ya nchi, pia nchini
Tanzania kuna baadhi ya kampuni zenye tabia ya kubadilisha majina mara muda wa
kuanza kulipa kodi kwa mujibu wa sheria unapo karibia, tabia ambayo inakosesha
serikali hela nyingi zitokana na kodi.Sina haja ya kutaja majina ya kampuni
zenyewe kwa sababu zinajulikana.
Ukijaribu kutadhimini huo uhuni wa kuficha hela kwa siri nje
ya nchi unaofanywa na vigogo wa
kitanzani na tabia ya kampuni kubadilisha majina yao mara kwa mara pale muda wa
kuanza kulipa kodi unapofika, Utagundua serikali ya Tanzania inapoteza mamilioni ya pesa kila
siku pasipo kuwa na sababu yoyote.
Ikiwa serikali haipokei hela kutoka mbinguni bali hutegemea
kodi yangu mimi na wewe ili kuweza kufanya shughuli zake kama vile kuboresha
elimu, afya, barabara na mambo mengine mengi, kwa nini wengine mnaficha hela
zenu nje ya nchi na kuikosesha serikali mapato? Labda mwenyewe utakuwa na jibu
kamili kuhusu hilo.
Kwa kuishia hapo kwa leo, Tanzania tuna nafasi ya kuimarisha
uchumi wetu na kuepukana na suala la kuombaomba kutoka nchi za Magharibi endapo
tutaacha urafiki na huruma usikuwa na tija kwa wahujumu uchumu. Kama mtu
anahofiwa kuihujumu uchumi wa nchi kwa kukwepa kulipa kodi, afanyiwe uchunguzi
wa kina bila kupepesa macho na kama akizibitika kuwa na kosa basi apewe adhabu
sitahiki kwa sababu itmfanye yeye kubadili tabia na pia itakuwa somo kwa
wengine wenye tabia kama hiyo.
0 comments:
Post a Comment