Nafikiri kama siyo genius basi ni gifted kwa aliye amua kuja na sera hii ya kuweka mipira ya kutumuia wakati wa tendo la ndoa (condoms) katika sehemu za kutolea huduma za jamii kama vile stendi za mabasi, nyumba za kulala wageni bila kusahau sehemu za kuendea haja ndogo na kubwa (public toilets).


Pichani ni box la 'condom' likiwa chooni katika moja ya chuo kongwe na maarufu hapa nchini.

Ni wazi kwamba suala la magonjwa ya zinaa hasa UKIMWI kwa muda mrefu imekuwa tishio duniani hususani kwa nchi zilizoko kusini mwa jangwa la sahara Tanzania ikiwa mojawapo, hivyo huduma hiyo ni muhimu sana!

Kwa takwimu zisizo rasmi kuhusu hali ya maambukizi ya ugonjwa UKIMWI dunia  ni kwamba, kati ya waadhirika milioni 34, asilimia 69 wanapatikana kusini mwa jangwa la Sahara. Kwa ujumla kuna jumla ya waadhirika wa ugonjwa wa UKIMWI milioni 23.8 katika bara la Afrika hadi sasa.

Kuhusu huduma hii ya 'condoms' katika sehemu zenye  mikusanyiko ya watu, mtandao huu umejaribu kuongea na mwanafunzi mmoja wa  Chuo cha uandishi wa habari na mawasiliano kwa uma  ya Chuo kikuu cha Dar es salaam amabaye hakupenda jina lake litajwe hadharani  ili kujua maoni yake kuhusu suala hilo na alikuwa na haya ya kusema.

'' Kwangu mimi naona bado huduma hiyo haitasaidia chochote katika harakati za kupambana na UKIMWI kwani tatizo siyo kwamba watu hawana 'condoms', tatizo ni kwamba watu hawana elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya kinga.....unakuta mtu anazo kinga nyumbani kwake laki bado hakumbuki kuzitumia coz hajapata elimu ya kutosha. Mimi nafikiri TACAIDS iwe na mazoea ya kuendesha mihadhara kuhusu matumizi ya kinga katika sehemu zenye mikusanyiko ya watu, wakifanya hivyo nadhani program yao hiyo itafanikiwa''.

(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top