Ikiwa ni siku chache mara baada ya kutupiwa virago vyake na  klabu ya Manchester United,  Davidy William Moyes aliamua kufunga safari yeye na mke wake Pamela na kuelekea huko katika fukwe za MIAMI nchini Marekani kujipa mapumziko mafupi kabla ya kuamua cha kufanya hapo mbeleni.

David Moyes
Moyes akiwa katika pozi na bibie Pamela huku akiwa bize na simu ishara ya kuweka mipango mingine ya baadaye baada ya kutupiwa virago na Man U
Ni wazi kwamba tangu Moyes atue dimbani Oldtrafford kuridhi mikoba ya Sir Alex Furguson Juni mwaka 2013 hajawahi kufurahia maisha ya pale kutokana na matokeo mabovu yaliyokuwa yakiandama klabu ya Mashetani wekundu, hususana rekodi mbaya ambazo zilikuwa zikivunjwa kila kukicha.

David Moyes Manchester United

Baaadhi ya rekodi mbaya zilizo ikumba Man U msimu huu chini ya David Moyes ni pamoja na kufungwa kwa mara ya kwanza na Swansea City huku timu zingine zikifanikiwa kuweka rekodi ya kuifunga Man U katika dimba lake la nyumbani baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa muda mrefu, mfano West Bromwich Albion ambayo haijawahi kuifunga Manchester United katika uwanja wake wa nyumbani tangu 1978 lakini ilifanikiwa kufanya hivyo msimu huu chini ya Moyes.

Baada ya Moyes kuanchia ngazi katika klabu ya Man U mnano  Aprili 21,2014 kufuatia kipigo cha magoli 2-0 dhidi ya Sunderlad huko dimbani Goodsonpark, klabu hiyo sasa iko chini ya mchezaji wake nguli Ryan Joseph Giggs amabye ana hudumu kwa muda wakati meneja mpya Louis Van Gaal akisubiriwa  kuja kukinoa klabu hiyo akiwa kama  Meneja mkuu.

Giggs amefanikiwa kukianza kibarua hicho kwa uzuri kabisa baada ya kumpa Norwich City kipigo cha mbwa koko cha magoli 4-0 kitendo kilicho wafurahisha wapenzi Man U kote duniani.




(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top