Mchezaji bora wa dunia mwaka 2014, Cristiano Ronaldo ameiomba serikali yake ya Ureno kumpa walinzi (mabodigadi) wa kutosha wa kumlinda saa 24 akiwa huko nchini Brazil. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail ni kwamba serikali ya Ureno imekubali kuandaa mabodigadi 6 kwa ajili ya timu yao ya taifa ambapo wanne kati ya hao ni wa mkali CR7!.
![]() |
CR7 |
Mahitaji mengine ni kama vile vyumba kulala wachezaji kuwekewa mfumo (system) zenye kutoa maji ya moto, hiili limependekezwa na wachezaji wa Japan, wakati huo huo wanandinga wa Ecuador wao wamependekeza kila siku wapatiwe japo tenga moja la ndizi kila baada ya mechi na hata wakiwa katika mazoezi.
![]() |
Hiki ndicho walichopendekeza wanandinga wa Ecuador |
Lakini kwa upande wao Colombia, Ugiriki, Ivory Cost pamoja na Japan wao wameomba nchi ya Brazil kuwapatia vijana wadogo wasiocheza soka la kulipwa kama 15 hivi ambao watakuwa wakichanganyana nao wakati wa mazoezi huko Brazil.
Huduma ya Tv na internet yenye kasi ndiyo huduma amabayo angalau kila nchi kati ya nchi 32 ilipendekeza kuwepo katika vyumba vya kulala wachezaji. Nchi zingine zilizofuzu kama vile Uingereza bado mapendekezo yao yanasubiriwa. (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment