Aprili 23, 2014  ni siku nyingine tena  ya kipekee kwa wanafunzi wa Shule kuu ya Uandishi wa habari na Mawasilano kwa Uma SJMC ya chuo kikuu cha Dar es salaam ammbapo walipata nafasi ya kukutana na kuzungumza naye mwandishi wa habari mkongwe na maarufu barani A frika na duniani kote, Dr. Shaka Ssali kutoka Voice of America (VOA).

Ssali amezungungumza mabo mengi sana ya msingi kwa waandishi wa hapari chipukizi chuoni hapo, machache kati ya hayo ni namna ya kufanikisha ndoto yako kwa kuamini katika kile unacho kifanya na kufanya kwa bidii nana kwa uaminifu wa hali ya juu.

Aliyekaa katikati ni Dr.Shaka Ssali ( mtoa mada) wa kushoto ni muhadhiri katika chuo cha uandishi wa habari  na mawasiliana kwa uma SJMC Dr.Ayub Rioba  na wa kulia ni Ass. Dean wa SJMC  Dr.Andindilile. 

"kama unataka kufanikiwa katika jambo lolote unalolifanya, basi fanya kwa bidii na kwa uaminifu wa hali juu na hapo lazima utaona matunda yake". Shaka Ssali alisema.

Aidha, wahadhiri mbalimbali chuoni hapo walionekana kuguswa na maneno aliyokuwa akinena Dokta huyo na wengine kuanza kuuliza maswali fulani fulani kuhakikisha mada inakuwa ya moto zaidi.

Aliyesimama ni Mr.Charles Irigo akijaribu kusisitiza kile alicho kuwa akizungumza Dr. Ssali.


Nao wanafunzi ambao ndiyo walikuwa walengwa wa mada yenyewe walikuwa makini zaidi kufuatilia kile alichokuwa akizungumza dokta huyo
Wanafunzi wa Sjmc wakisilikiliza kwa makini kile alichokuwa anazungumza Shaka Ssali.
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo akiuliza swali kwa Ssali, pembeni upande wa kulia ni Mr Katunzi, mhadhiri katika shule ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa uma.


**Picha zote na Francis Kivuyo***
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top