Kocha wa Nigeria Stephene Keshi amejiuzulu wadhfa .ke katika timu ya taifa ya Nigeria.
Keshi amejiuzulu punde baada ya timu ya Super Eagles kuondolewa kutoka
kwenye kipute cha kombe la dunia ilipolazwa 2-0 na Ufaransa.
![]() |
Stephen Keshi |
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alichukuwa wadhfa huo mwaka wa
2011 na akaiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa afrika mwaka uliopita .
Nahodha wa timu hiyo Joseph Yobo aliyejifunga bao la pili la Ufaransa naye
pia ametangaza kustaafu .
![]() |
Nahodha wa Nigeria, Joseph Yobo (jezi ya kijani) aliyojifunga bao 2 na kulizamisaha jahazi mazima. |
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Keshi kujiuzulu wadhfa wakae,mwaka wa
2013 Keshi alikuwaradhi kujiuzulu lakini akashawishiwa kusalia kama kocha
na waziri wa michezo wa Nigeria.
Chini ya uongozi wake Super Eagles imefuzu kwa mara ya kwanza katika
mkondo wa pili wa kombe la dunia tangu mwaka wa 1998 licha ya kukumbwa
na migomo ya mara kwa mara ya wachezaji wake wakidai malimbikizi ya
marupurupu yao.
Kuondoka kwake kumefikisha idadi ya wakufunzi waliojiuzulu kufuatia
matokeo duni katika kombe la dunia kutimia makocha 6.
Makocha wengine waliondoka ni pamoja na Luis Suarez, wa Honduras, Carlos
Queiroz wa Iran's , Alberto Zaccheroni wa Japan , Cesare Prandelli wa italia
na Sabri Lamouchi wa Ivory Coast.
Keshi, aliwahi kuhudumu kama kocha wa Mali na Togo.
0 comments:
Post a Comment