Aliyekuwa kocha msaidizi katika klabu ya Wanazambarau kutoka
jijini Mbeya, Mbeya City Fc bwana Maka Malwisyi amelamba "dume" na
sasa ni kocha mkuu kunako klabu ya Panone Fc ya mkoani Kilimanjaro inayoshiriki
ligi daraja la kwanza.
![]() |
Kocha mkuu Panone Fc, Maka Malwisyi |
![]() |
Maka Malwisyi mara baada ya kukabidhiwa ofisi kama kocha mkuu wa panone FC ya huko mkoani Kilimanjaro,July 21-2014 |
"Baada ya mkataba wangu kufika mwisho
na Mbeya City Fc, nilisema wazi kabisa kwamba siko tayari kuongeza mkataba mpya
kwa sababu hivi juzi mwezi mei nimetoka kuchukua leseni B ya ukocha katika
programu maalumu ya makocha iliyoendeshwa na makocha wa kimataifa hapa nchini chini
ya TFF na kiukweli kwa sasa naona ni vyema na mimi kupata timu ya
kuifundisha kama kocha mkuu ili uwezo wangu nilionao uonekane" Malwisyi
alisema wakati akilonga na mishemishezamtaa.blogspot.com.
Maka Malwisyi ni miongoni mwa makocha
wanotajwa kuwa na mchango mkubwa wakati akiwa na klabu ya Mbeya City. Akiwa na
klabu hiyo, Malwisyi na kocha mkuu wa klabu hiyo kwa sasa, Juma Mwambusi,
waliipandisha Mbeya City FC katika ligi
kuu Tanzania Bara msimu wa 2013/2014 ambapo timu hiyo ilikuwa moto wa kuotea
mbali hususani kwa timu kongwe nchini kama vile Simba Sc na Dar Young A
fricans.
Maka Malwisyi alianza kibarua chake hicho kipya tangu July 21 mwaka huu na amesema anafurahia
kuwa sehumu ya Panone FC kwani falsafa za timu hiyo zinafafana na falsafa zake.
Malwisyi amesema wana-Panone fc wategemee makubwa klabuni hapo kwani amekuja
kuleta mapinduzi chanya katika klabu ya Panone na soka la Tanzania kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment