Fifa imetupilia mbali rufaa ya Fc Barcelona ya kutokufungiwa kusajili kwa misimu miwili ijayo.Kwa mujibu wa ripoti ya shirikisho la kandanda duniani FIFA inasema hukumu ya hiyo ya Barcelona itaaanza kufanya kazi rasmi kuanzia Januari 2015 hadi 2016.

Manchester City v Barcelona - UEFA Champions League Round of 16

Kwa maana hiyo sasa Wakatalunya hawatakuwa na nafasi yoyote  ya kufanya usajili wowote wa kitaifa wala wa kimataifa, wakati huo huo FIFA imeimuru Barcelona kulipa faini ya Uro milioni 295000 ikiwa ni sehemu ya adhabu hiyo.

Adhabu ya Barcelona ya kutosajili kwa muda wa misimu miwili imesebabishwa na wao kuvunja sheria za usajili kwa kuwasajili  wachezaji wenye umri chini ya miaka 18 kinyume cha sheria. Hata hivyo Barcelona wamesema wanajipanga kukata rufaa nyingine ya juu katika mahakama ya juu ya soka duniani (Cort of Arbitration for Sports).

  (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top