Bingwa mtetezi wa liki kuu Tanzania Bara, Azam FC ameaga rasmi michuano klabu bingwa CECAFA-Kagame Cup msimu wa 2014 baada kutolewa kwa mikwaju ya penati na klabu ya Al-Merreikh kutoka Sudan ikiwa ni hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.
Hadi dakika tisini za mpepetano huo zinamalizika, siyo Azam wala Al Merreikh iliyofanikiwa kupata goli, kama kawaida timu zote zilikwenda katika dakika za nyongeza lakini milango bado iliendelea kuwa migumu kwa pande zote kitu kilicholazimu kutumia mikwaju ya penati kuamua mshindi katika mtanange huo.
Kama amabavyo inafahamika na kuaminika kwa wengi kuwa peneti haina fundi, basi Al-Merreikh iliweza kubahatisha na kufanikiwa kupata penati 4 huku wapinzani wao, Azam Fc wakiambulia penati 3 pekee. Mchezo huo ulifanyika katika dimba la Nyamirambo.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment