Na mwandishi wetu, Tanga

TIMU ya Coastal Union alimaarufu kama "wagosi wa ndima" ya jijini Tanga kesho Agosti 19 mwaka huu inatarajiwa kuondoka mkoani humo kuelekea Visiwani Pemba kwa kutumia usafiri wa Ndege kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki mbili kwa ikiwa ni harakati za  kujinoa kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu sokaTanzania bara itakayoanza mwezi Septemba 20 mwaka huu.

View photo in message
Wagosi wa  Ndima wameamua kufuata nyao za timu kongwo za hapa nyumabni, Simba Sc na Yanga Sc kwa kwenda kunolea makali yao visiwani.

Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa timu hiyo itaondoka kesho saa tatu asubuhi kwenye uwanja wa Ndege jijini Tanga ikiwa  na msafara wa wachezaji 28 na viongozi sita. Assenga amesema kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kufanya mazoezi yake kwenye viwanja vya migombani visiwani humo asubuhi na jioni wakiwa na lengo kuu la kuhakikisha wanajiandaa vema na michuano ya Ligi kuu soka
Tanzania bara.
Aidha, benchi la ufundi la Costa Union  katika msafara huo litakuwa likiongozwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Yusuph Chippo, Msaidizi wake Benard Mwalala, Kocha wa makipa Razack Siwa na daktari wa timu na mtunza vifaa. (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top