Baada ya kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa Swansea City, Luis Van Gaal alianza kupiga mahesabu wa nani wa kutolewa kafara kunako Old Trafford ili kutoa nafasi kwa usajili wa wanandinga wapya.
Wachezaji waliotajwa kuhusika katika kafara hiyo mara baada ya mechi dhidi ya Swansea Jumapili ya Agosti 17 mwaka huu ni Luis Nani, Anderson pamoja na Wilfed Zaha, ambapo mpaka sasa hivi wanandinga hawa hawashiriki katika mazoezi ya kila siku na kikosi cha kwanza cha Van Gaal, wao hufanya mazoezi yao wenyewe baada ya kikosi cha kwanza kumaliza.
Mpaka sasa zoezi la kafara limeanza kufanya kazi, hii ni baada ya magazeti ya leo ya huko Ulaya kuonyesha kuwa kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi, Luis Van Gaal yuko tayari kabisa kumtoa winga wake Luis Nani pamoja na kitita cha Uro milioni 16 ili kumnasa beki wa kati wa timu ya Taifa ya Argetina na klabu ya Sporting Lisbon, Faustino Marcos Alberto Rojo mwenye umri wa miaka 24.
![]() |
Ushindi wa jana wa Chelsea wa magoli 3-1 dhidi ya Burnley pamoja usaji wa Man U ndiyo habari ya mjini katika mitaa mbalimbali huko Ulaya. |
Mchezaji mwengine ambaye yuko mbioni kujiunga Mashetani wekundu muda wowote kuanzia sasa ni mshambuliaji wa Real Madrid Angel De Maria.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment